Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Na Baraka Kizuguto,Dar es salaam
Mechi ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika kati ya Young Africas dhidi ya timu ya FC Platinum ya Zimbambwe iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam iliingiza mil 91,660,000 kutokana na watazamaji 14,563 waliokata tiketi kushuhudia mchezo huo.

Mgawanyo wa mapato katika mchezo huo ni, VAT 18% sh. 13,982,033, Gharama ya tiketi sh. 12,380,000, Uwanja 15% sh. 9,794,694.92, Gharama za mchezo 15% sh. 9,794,694.92, TFF 5% sh. 3,264,898.31, CAF 5% sh. 3,264,898.31 na Young Africans 60% sh.39.178,779.66

Wakati huo  Ligi Kuu ya Vodacom inatarajiwa kuendelea kesho (jumatano) kwa viwanja vitatu kutimua vumbi, Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Young Aricans watawakaribisha Kagera Sugar mchezo utakaoanza majira ya saa 10 kamili jioni.

Jijini Tanga maafande wa Mgambo Shooting watakua wenyeji wa Simba SC katika mchezo utakaofanyika uwanja wa Mkwakwani, huku jijini Mbeya wenyeji Mbeya City watawakaribisha timu ya ya Stand United kutoka mkoani Shinyanga kwenye uwanja wa Sokoine.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top