Na Anitha Jonas – MAELEZO,Dodoma.
Serikali inatarajia kuanzisha Baraza la Vijana litakalo kuwa chombo cha vijana
kitakacho waunganisha Kitaifa bila kujali itikadi zao za Kisiasa,Imani zao za Kidini wala
tofauti zao za Rangi,hayo yamesemwa na Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na
Michezo Mhe.Fenella Mukangara alipokuwa akisoma Muswada wa Sheria ya Baraza la
Vijana Tanzania Bungeni Mjini Dodoma.
Mheshimiwa Mukangara aliendelea kusema Baraza hilo litaisaidia Serikali kuweza
kuwafikia vijana kwa urahisi na kusikiliza shida zao pamoja na kutoa ufumbuzi wa hoja
mbalimbali za vijana.Hata hivyo chimbuko la Muswada huo ni katika kutekeleza Sera
ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana ya 2007,Ibara ya 3 Sehemu ndogo ya 11 inayosema
kwa uwazi Serikali itawezesha kuundwa kwa Baraza Baraza la Vijana na kuanzisha
mfumo wa kisheria ili kuliwezesha kufanya kazi.
“Madhumuni ya Muswada huu ni Kutunga Sheria ya Baraza la Vijana Tanzania(The
Youth Council of Tanzania 2015) ili kuwa na chombo cha Kitaifa cha kuwewezesha
vijana kujadili masuala yao,kutambua majukumu yao,kukuza maadili mema,kukuza
moyo wa umoja ,uzalendo,uwajibikaji na kujitolea kwa malengo chanya miongoni mwao
katika nchi yetu,”alisema Mhe.Mukangara.
Mbali na hayo katika sehemu ya pili kifungu cha 4-15 cha Muswada huo unaeleza juu
ya masharti mbalimbali kuhusu Uanzishwaji,Uanachama,Muundo na kazi za Baraza.Pia
sehemu hii imefafanua Mamlaka ya Baraza na vyombo vya utendaji katika ngazi ya
Taifa,Mkoa na Wilaya.
Aidha,kwa upande wa maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii
yaliyosomwa na Mwenyekiti wake Said Mtanda aliishauri Serikali katika kifungu cha
4(3)Kisomeke Uanachama utakuwa na uwazi na hiari kwa kijana yeyote mwenye umri
wa kuanzia miaka 15 mpaka 35.Pia kifungu cha 4(4) imeeleza kuwa baraza halitakuwa
kisiasa liongezwe neno halitakuwa na Itikadi za Kidini.
Katika kipindi cha majadiliao ya Muswada huo naye Mhe.Kuluthum Mchuchuri (Mb) Viti
Maalum CUF aliipongeza Serikali kwa mchakato wake mzuri wa kuandaa Baraza la
Vijana litakalo saidia vijana kujadili matatizo yao na kuyawasilisha Serikali kwa kupatiwa
ufumbuzi kwa urahisi,pia ameishauri Serikali katika suala la wajumbe uwawakilishi
waanze kuanzia ngazi ya Kata na Serikali pia iweke wazi ni kwa utaratibu gani
wawakilishi hao watapatikana.
Naye Mhe.Magret Sitta Mbunge wa Viti Maalum CCM aliiomba Serikali kuandaa ziara
kwenda kuangalia mabaraza ya Vijana katika nchi za wenzetu yanafanyaje kazi na
kujifunza,pia aliendelea kuiomba Serikali itoe mafunzo mbalimbali ya ufundi kwa
kushirikia na taasisi ya Veta na Vyuo vya Wananchi ilikuwapatia elimu itakayo wasaidia
vijana kujikwamua kiuchumi na kupunguza idadi ya vijana wa vijiweni.
Pamoja na hayo naye Mbunge wa Kasulu Mjini (NCCR) Mhe.Moses Machali alishauri
Serikali Kuanzisha asasi moja ambayo vijana watakayo jiunga huko ili kudhibiti
uanzishwaji wa asasi bandia kwa watu wenye nia ya kujinufaisha,pia aliipongeza
Serikali kwa kuleta Muswada huo kwani unamanufaa Makubwa kwa vijana.
Aidha,mbali ya kuwepo na marekebisho mbalimbali ya Muswada huo Serikali iliyapokea
maombi ya Suala la Baraza hilo kuanzia katika ngazi ya Kata ilikupata uwakilishi
uliyowa uhakika na baraza likalete manufaa kwa kuanzia ngazi ya chini ambapo ndipo
vijana wengi wanapatikana na jamii inawafahamu kwa usahihi zaidi.
Halikadhalika Serikali iliridhia kuanzishwa kwa uwakilishi wa vijana watano kutoka kundi
maalum kwa maana ya wenye ulemavu na ili kuweka uwianao wa vijana hawa kuweza
kuwasilisha maombi yao kwa Serikali kwa urahisi huku ikizingatia mahitaji yao maalum.MICHUZI MATUKIO
Post a Comment