Kuelekea mchezo
wa michuano ya kombe la shirikisho barani afrika kati ya Yanga dhidi ya Etoile
Du Sahel ya Tunisia utakaopigwa jumamosi hii April 18 katika uwanja wa taifa,Chama
cha soka mkoa wa Dar es salaam DRFA,kimeitabiria makubwa klabu hiyo ya Jangwani
kuvuka katika kizingiti hicho kigumu kwa mchezo wa nyumbani na ugenini dhidi ya
wababe hao wa Tunisia.
Mwenyekiti wa
chama hicho Almasi Kasongo,amesema ili yanga ifanye vizuri katika mechi hiyo na
kuwapa raha mashabiki wake na watanzania kwa ujumla,ni lazima icheze kwa uangalifu
mkubwa na kukwepa kuendana na style ya kupoozesha mpira wanayoitumia wapinzani
katika mechi za ugenini.
kasongo amelishauri
benchi la ufundi la Yanga chini ya makocha Hans Pluijm na msaidizi wake Charles
Mkwasa,kutumia mbinu ya kushambulia kwa muda wote ili kuwaduwaza wapinzani
ambao wakati mwingine hutumia mbinu ya kufanya mashambulizi ya kushtukiza.
Ametoa wito pia
kwa mashabiki wa soka mkoa wa Dar es salaam na maeneo ya jirani, kujitokeza kwa
wingi siku ya jumamosi kuishangilia Yanga ambao wanaliwakilisha taifa katika
mashindano hayo ya vilabu barani afrika.
Hata hivyo
DRFA inaamini kuwa Yanga ambayo ni moja ya timu zake zilizopo katika mkoa wa
Dar es salaam haina sababu ya kutofanya vizuri katika mchezo huo, kutokana na kuwa
na kikosi kizuri kilichovisambaratisha katika michuano hiyo vilabu vya BDF ya
Botswana pamoja na Platinum ya Zimbabwe.
Imetolewa na Chama Cha Soka Mkoa wa
Dar es salaam,DRFA.
Omary
Katanga,Mkuu wa Habari na
Post a Comment