Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi |
Na
Emanuel Madafa,Mbeya
WATU
19 wamepoteza maisha papo hapo na wengine wawili kujeruhiwa katika ajali ya gari
ndogo la abiria Toyota Hiace baada kushindwa kukata kona na kugonga gema kisha
kutumbukia mtoni kwenye eneo la Uwanja wa ndege lililopo katika Kata ya Kiwira
Wilayani Rungwe, Mkoani Mbeya.
Tukio
hilo limetokea leo saa 3:00
asubuhi ambapo ajali hiyo ilihusisha gari ya abiria aina ya Hiace yenye
namba za usajili T290 ADU iliyokuwa ikitokea Jijini Mbeya kwenda Kiwira ikiwa
imebeba wafanyabiashara ambao walikuwa wanakwenda kwenye mnada uliokuwa unafanyika
mjini Kiwira Wilayani Rungwe.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi,
amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba waliokufa ni watu 19 na kujeruhi
watu wawili akiwemo dereva na kondakta wa gari hiyo na kwamba wamelazwa katika
hospitali ya Igogwe iliyopo Wilayani Rungwe.
Aidha, Msangi amesema miili ya marehemu hao imehifadhiwa
katika hospitali ya Igogwe iliyopo Wilayani Rungwe na kuwataka wananchi
kujitokeza kuwatambua.
Akielezea
chanzo cha ajali hiyo,Kamanda Msangi, amesema ajali hiyo imetokana na mwendokasi
aliokuwa nao dereva wa Hiace, kwani inasemekana kwamba alikuwa akiwakimbia
madereva wa basi aina ya Coaster zinazofanya safari zake za Mbeya-Kyela na
Rungwe ambao wapo kwenye mgomo.
Amesema,
dereva huyo ambaye jina lake halikuweza kufahamika, akiwa katika mwendokasi
aliweza kuipita kona ya kwanza iliyopo kwenye eneo hilo la tukio ambalo linamteremko
mkali na alipofika kwenye kona ya pili gari ilimshinda na kugonga gema, kisha
kutumbukia kwenye mto Kiwira.
Akizungumza
na blog hii mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo aliyekuwepo katika eneo la kituo cha mabasi
cha NaneNane kilichopo Jijini hapa, Jofrey Gasper , alisema kuwa mgomo huo wa Coaster umetokana na baadhi yao kuzipinga
taratibu na sheria za usalama wa barabarani, na kwamba siku hiyo kulikuwa na
mwenzao ambaye alikamatwa na kutozwa faini ya shilingi 250,000 kutoka SUMATRA.
Inadaiwa,
kwamba wakati madereva hao wakiwa kwenye gari hiyo ndogo, wakiifukizia Haice,
dereva huyo alipata taarifa hivyo aliongeza
kasi ya gari, ndipo ilipomshinda alipofika kwenye eneo la kona lenye mteremko
mkali na kisha kutumbukia mtoni.
Mwisho.
Post a Comment