Ajali za barabarani hazipaswi kuonekana kama
jambo la kawaida. Kusafiri kwa basi hakupaswi kulinganishwa na kujitoa muhanga.
Nilipendekeza:
1. Kuwe na taasisi mpya ya "Highway
Patrol" yenye magari ya kutosha na askari waadilifu. Traffic kuwa na
vijiwe mahsusi barabarani haisaidii.
2. Magari ya abiria yawe na kifaa ambacho
kinatoa mlio mkali ndani ya basi spidi inapozidi na kutuma automatic SMS kwenye
namba Maalum polisi.
3. Highway Police wawe wanazunguka barabarani
kila wakati badala ya kuwa na geti tu au kijiwe cha kupumzika.
4. Iwapo ajali itapatikana kutokana na ubovu
wa basi, leseni ya kampuni ya mabasi isimamishwe. Hii itawafanya wenye mabasi
wawe makini.
5. Magari yanayoharibika barabarani hayapaswi
kupaki highway siku tatu yanapaswa kupewa masaa matatu kutengenezwa au
kuondolewa barabarani.
6. Mamlaka ya usimamizi wa Usalama Barabarani
kati ya SUMATRA na Polisi yabainishwe wazi ili kuwe na uwajibikaji.
7. Huduma za dharura za uokoaji wakati wa
ajali, ikiwemo uwepo wa helikopta, ni muhimu, na hii iende sambamba na
kuboresha huduma katika hospitali zetu. Watu wengine hufa kwa kuvuja damu
nyingi tu.
8. Ujenzi wa barabara, kwa maana ya upana wa
barabara, mabega na madaraja na alama na ishara za barabarani ni muhimu ukawa
wa viwango.
9. Anapokamatwa dereva anayeendesha kwa
uzembe, leseni yake isimamishwe papo hapo. Akiwa amelewa asiruhusiwe kuendesha
tena gari la abiria.
10. Ndani ya basi, au kwenye tiketi, kuwe na
namba za simu za kupiga au kutuma ujumbe Polisi abiria wakiona uendeshaji wa
dereva hauridhishi.
Post a Comment