Ikiwa
ni miaka mitatu sasa imepita tangu aliekuwa staa wa Bongo Movies,
marehemu Steven Kanumba, inadaiwa kuwa gari alilokuwa akilitembelea aina
ya Toyota Lexus lenye namba za usajili T750 AER limezidi kudoda sokoni.
Kwa mujibu wa chanzo makini cha gazeti la Risasi kimepenyeza habari
kuwa gari hilo lililonunuliwa na marehemu kwa shilingi milioni 78,
linapatikana maeneo ya Msasani, jijini Dar kwenye jengo la mikopo ambapo
linauzwa kwa bei chee ya shilingi milioni 18 hadi 14.
“Nilikuwa nikijipitia kukagua magari lakini ghafla nikakutana na gari
la Kanumba. Sikuamini mpaka pale nilipoingia na kulipiga picha kisha
nikaambiwa na thamani yake,” kilisema chanzo.Chanzo kiliendelea
kutiririka kuwa huenda kuna mkopo ulichukuliwa na kuacha dokumenti zote
za gari hiyo na iliposhindikana kulipwa gari hiyo ikapigwa mnada.
“Sidhani kama gari kali kama ile ipigwe bei ya milioni 18 tu, lazima
kutakuwa na mkopo ambao haujamalizwa ndiyo maana limepigwa kiasi hicho
cha pesa ili kukamilisha.”Awali ilisemekana kuwa gari hilo lilikabidhiwa
kwa msanii wa filamu Bongo, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ ili alinunue kwa
gharama ya shilingi milioni 40 lakini kwa kuwa liligundulika na matatizo
mengi akawa tayari kutoa shilingi milioni 25 ambapo pia ilishindikana
na kurudishwa kwa familia ya Kanumba.
Gazeti hilo lilimtafuta mama Kanumba, Flora Mtegoa ili kujua
anazungumziaje gari hilo kudoda sokoni, alijibu:“Mimi sijui chochote
kuhusu hilo gari naona mnazidi kuniumiza tu hapa naumwa, hata kama
nimeuza au limefanywaje jamani maswali mengine yanaumiza hebu niacheni
maana sijui kinachoendelea kuhusu hilo gari,” alisema Mama Kanumba.
12.04.2015 - Tags:
KANUMBA CREDIT BONGO MOVIE
Post a Comment