Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho Richard Mbwaga |
kaka wa marehemu Ally Kandonga |
Na
Saimeni Mgalula,Mbeya
Mkazi mmoja Jaisoni Mwandenga (55) wa Mtaa wa Nero uliopo kata ya
Kaloleni Wilaya ya Momba Mkoani hapa,ameuawa kikatili nyumbani kwake
kwa imani za kishirikina na watu wasiofahamika na kisha kupasuliwa
kichwani na kutobolewa mgongoni kwa kutumia silaha aina ya sululu .
Akizungumzia Tukio hilo la kikatili Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho
Richard Mbwaga alisema Mwandenga aliuawa majira ya saa 8:30 za usiku
mwaka huu nyumbani kwake mpande ambako ndio anakofanyiaga shughuli
zake za kilimo.
Alisema kuwa Watu hao wanyama walitumia njia ya kuvunja mlango na
kuingia ndani ambapo walimkuta akiwa amelala kisha kumpiga kichwani na
kuumwaga ubongo wake kisha kummalizia sululu sehemu ya mgongo mbayo
waliicha sululu mpaka jeshi la polisi lilivyokuja kuichomoa na
kusababisha mauti hao yamkute ,alisema Afisa mtendaji .
Aliendelea kwa kusema kuwa chanzo cha mauaji hayo ni marehemu
kusadikika kuwa ni mchawi kwa kuwaloga wenzake kwa yeye anapata mazoa
mengi kuliko wenzake kitu ambacho kimepelekea kuhisiwa kuwa ni
mshirikina na ndo sababu kubwa ambayo imempa umauti Jaisoni,alisema
Richard.
Hata kaka wa marehemu ambaye alijitambulisha kwa
jina la Ally Kandonga alisema kuwa yeye alipigiwa simu mida ya saa
2:00 asubuhi kuwa kaka yenu ameua kikatili.
Alisema mara baada ya kupigiwa simu nilifunga safari mpaka nyumbani
kwake Huko Mpande ambako nako amejenga kwajili ya kupumzika pindi
anapokuwa anafanya shughuli zake za kilimo huku na nero akiwa
ananyumba ya kuishi.alisema Ally
Kandonga alisema akijaribu kuvuta taswila mara ya kwanza marehemu
alinusurika kufa kwa kukatwa katwa na Mapanga tukio ambalo lilimfanya
marehemu kuwa haongei kutokana na kujeruhiwa sehemu za mdomoni
,alisema Kandonga ,
Aliendelea kwa kusema kuwa hali hiyo ya kuwa haongei iliwafanya ndugu
kutokujua kuwa marehemu anatatizo gani na baadhi ya wananchi kutokana
na kuwa bubu kitu ambacho ndugu walimkatalia kuwa kwenda tena mpande
lakini yeye aliwakatalia ndugu zake na kurudi tena ambapo ndo Alikofia
huko.alisema ally.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kaimu kamanda wa polisi mkoa wa
Mbeya Ahmed Msangi ambaye alitoa wito kwa jamii kuacha kuchukuwa hatua
mkononi na wawe na kasumba ya kuwafikisha sehemu husika ili
kuwachukulia hatua za kisheria na sio kuchukuwa maamuzi yao ya kufanya
mauaji hayo kwani ni kinyume na sheria.
Aidha aliendelea kutoa wito kwa watu ambao wanafahamu watu waliofanya
unyama huo watoe taharifa ili watu hao wakamatwe na kuchukuliwa hatua
za kisheria kwa mujibu wa jeshi la polisi na mara baada ya hayo jeshi
la polisi lilichukuwa mwili wa maremu na kuifadhi katika hospitari ya
serikali Mjini tunduma kwaajili ya uchunguzi.
MWISHO:

Post a Comment