Na Baraka Kizuguto,Dar es salaam
Kamati ya Rufaa ya Nidhamu - TFF imekutana leo
tarehe 12/04/2015 kujadili rufaa No. 1/2014 ya DR. DAMAS NDUMBARO dhidi ya TFF.
TFF iliwakilishwa na Wakili Msomi Emmanuel Muga na
Dr. Ndumbaro hakufika wala hakuwakilishwa na wakili wake.
Kufuatia kutofika kwa Dr. Ndumbaro, Kamati, kwa
Azimio moja, iliamuru TFF itoe wito mpya na
mpaka tarehe 14/04/2015 uwe umemfikia Dr. Ndumbaro, ukimfahamisha tarehe
ya kikao kijacho cha kusikiliza rufaa yake.
Imetolewa na Mwenyekiti,
|
Post a Comment