Kampuni ya Google imatangaza kuwa
itazindua huduma mpya nchini Marekani ambayo inaweza kutumiwa nyumbani
na wakati wa safari za mataifa ya kigeni.
Huduma hiyo inayo fahamika kama Project Fi inatapatikana kwa simu za Smartphone za Google Nexus 6.
Huduma
hiyo itatumia maeneo yaliyo na Wi-Fi sambamba na huduma zingine za
mawasilianoi nchini Marekani za Sprint na T-Mobile na inaweza pia
kutumiwa kwenye nchi 120 bila malipo ya ziada wakati mtu anaposafiri nje
ya nchi.
Huduma hiyo itatolewa kwa malipo ya dola ishirini kwa
mwezi kwa huduma za kawaida na dola kumi kwa mwezi kwa kila gigabyte ya
data inayotumika.
Google inasema kuwa huduma hiyo huwa inajiunga
moja kwa moja na zaidi maeneo milioni yenye huduna za Wi-Fi na mteja ana
uwezo wa kuhamiswa kutoka kwa mtandao mmoja hadi mwingine kulingana na
ni upi unaotoa huduma bora zaidi
Post a Comment