Kufuatia tatizo la kushindwa kupata ujauzito alilonalo
msanii maarufu Bongo, Wema Sepetu, hivi karibuni waganga wapatao 26
kutoka sehemu mbalimbali nchini walijitokeza na kuomba kuunganishwa na
staa huyo ili wamtibu.
Waganga hao wa tiba asilia pamoja na madaktari kutoka hospitali
mbalimbali kwa nyakati tofauti walililipigia simu gazeti hili na kueleza
kuwa, wanashangaa kuona Wema anakosa amani wakati wao wanaweza kumtibu
na kuweza kuitwa mama kama wenzake.
“Unajua wapo wanawake ambao wanakosa amani kwa mambo ambayo
hawastahili, hili la Wema kutopata mtoto linatibika, mpeni namba yangu
kisha anitafute,” alisema mmoja wa wataalam hao aliyeomba jina lake
lisiandikwe gazetini.
Katika kujua Wema anapokeaje ofa aliyopewa na waganga hao, alitafutwa na alipopatikana alikubali mara moja kutibiwa tatizo alilonalo lakini akatoa angalizo.
Katika kujua Wema anapokeaje ofa aliyopewa na waganga hao, alitafutwa na alipopatikana alikubali mara moja kutibiwa tatizo alilonalo lakini akatoa angalizo.
“Kuna watu wengi sana ukiacha ambao wamejitokeza kwenu, mimi nina
meseji zaidi ya 400 ambazo nimetumiwa kwenye namba yangu ya WhatsApp na
simu kibao nimepigiwa watu wakijitolea kuja kushughulikia tatizo langu,
kiukweli kabisa nipo tayari.
“Lakini ni vizuri wakati naanza kutibiwa tayari nikawa na mwenza
wangu ambaye tutakuwa tumekubaliana na pale tatizo litakapoisha, iwe
rahisi kuzaa mara moja,” alisema Wema.
GPL
Post a Comment