Wananchi wakijaribu kuokoa mali zilizopo katika maduka hayo.Picha na Saimen Mgalula |
Kikosi cha Zimamoto kwa kushirikiana na wananchi wa eneo hilo kuuzima moto huo ambao umetekteza maduka zaidi ya Manne katika eneo hilo Mtaa wa Unyamwanga Kisimani mjini Tunduma. |
Na Mwandishi wetu,Mbeya
MOTO mkubwa umeteketeza
maduka zaidi ya Manne katika mtaa wa Unyamwanga Kisimani Mjini Tunduma
mkoani Mbeya April 19 mwaka huu.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa
Mbeya Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa moto huo
ulitokea saa 2 usiku mtaa wa unyamwanga ambapo maduka hayo
yaliyoteketea yalikuwa katika jengo moja
linalomilikiwa Albart Ndembwike mkazi wa Tunduma .
Kamanda Msangi amesema moto huo ulitokea katika moja ya duka kati ya
hayo Manne yaliteketea kwa moto ambapo chanzo chake bado hakijafahamika mara
moja ambapo uchunguzi wa tukio bado unaendelea .
Amesema changamoto kubwa
iliyopo katika eneo hilo LA Mji wa Tunduma ni ukosefu wa gari la zima moto hivyo katika tukio la
jana walilazimika kuomba msaada kwa majirani zao Zambia ambao walifika mara
moja na kuuzima moto huo kwa kushirikiana na wananchi wa eneo hilo.
Amesema changamoto hiyo
inatokana na wananchi wenyewe kufanya uhalibifu katika gari la zima moto
lililokuwepo katika mjini huo ambalo lilihalibiwa vibaya kwa kutupiwa mawe
kipindi nyuma ambalo kwa sasa lipo katika matengenezo.
Aidha jeshi la polisi
limelaani mtindo unaoota mizizi hivi sasa wa wananchi kujichukulia sheria
mkononi kwani kwa kufanya shambulio kwa kikosi cha zima moto mara kinapo wasili
katika eneo la tukio.
Amesema mashambulio ya aina
hiyo yamekuwa yakisababisha hasara ikiwa ni pamoja na kuvunjwa vioo vya gari,
kupotea kwa vitendea kazi pamoja na baadhi ya askari wa zimamoto kujeruhiwa
kitendo ambacho kinavunja moyo kwa askari hao.
Aidha mashuhuda wa tukio
hilo wanaeleza kuwa moto huo ulishika kasi kwa haraka kutokana na hali ya hewa
kuwa ya upepo mkali licha ya juhudi za wananchi kuuzima lakini uliwashinda
nguvui hadi pale kikosi cha zima moto kutoka nchini Zambia kilipo fika na
kuuzima moto huo.
Mwisho.
Post a Comment