Rais wa TAFF Mwakifwamba akiwa na Jack na Tico baada ya kuwapatanisha |
Baada ya kutengana kwa muda mrefu hatimaye leo hii magwiji wawili
katika tasnia ya filamu Jackson Kabirigi ‘Jack’ na Timoth Conrad ‘Tico’
wamepatanishwa na Shrikisho la filamu (Taff) baada ya mazungumzo
yaliyochukua saa kadhaa hadi kufikia muafaka na kurudi kama mwanzo
iliyvyokuwa Timamu Effect.
Akiongea na mara baada ya tukio hilo John Kallaghe amesema kuwa
amefurahishwa na kazi kubwa iliyofanywa na Rais wa Taff Simon
Mwakifwamba kwa kutumia hekima zake na kumaliza tofauti iliyopelekea
kujenga Uhasama wa kimanenoa kati ya wasanii hawa walioitangaza Tanzania
kwa filamu yao ya Mdundiko.
“Moja ya kazi kubwa ambayo inabidi ifanywe na shirikisho ni kujenga
umoja kwa wadau wake ambao ni wasanii pamoja na watayarishaji kwa ujumla
wake, leo Tico na Jack kupatana na kurudi kufanya kazi pamoja tasnia
itasonga mbele,”anasema Kallaghe.
Tico naye amesema kuwa anaamini kuhusu ushirikiano wao ambao unaweza
kuleta tija katika utendaji wa kazi na anafahamu kuwa wanahitaji kuwa
pamoja lakini sababu kubwa ni wapambe ambao walifanikiwa kuwafanya wawe
mbali bila hata ya kujua ugomvi wao na kuiacha kampuni.
“Bongo Movie fitina ni nyingi sana msipokuwa imara mnageuka na kuwa
maadui bila sababu ya msingi naamini kuhusu kolabo yangu na Jack nadhani
naye ananihitaji kama ninavyomhitaji mimi sasa ni kazi hakuna maneno
tena,”anasema Tico.
Kila mtu anajisikia faraja kuweza kutatua tatizo hili ambalo lilikuwa
linaua tasnia ya filamu au kujenga pengo katika utendaji wa watu hawa
wawili vijana wadogo wenye ndoto za kufanya kazi kimataifa na ubora wa
juu, Jack mahiri katika uongozaji na Tico hatari sana katika
utayarishaji effects.
“Nimefurahia kuwepo na ndugu yangu Tico tulikuwa na ndoto kubwa sana
naamini ilikuwa kama likizo sasa tunarudi napenda kuwaahidi uongozi wa
Taff na funs wetu kazi zile kutoka kwa Tico chini ya Director Jack
zitashuka na kutikisa,”anasema Jack.
Naye Mwakifwamba amsema amefurahishwa sana na wasanii hao kuwa kitu
kimoja kwani moja ya changamoto kuwa inayosumbua katika tasnia ya filamu
ni hali ya wasanii na watendaji kujikuta wakiingia katika uhasama ambao
haujengi bali kubomoa umoja ambao unahitaji sana.
“Mimi kama kiongozi si kiongozi wa kukaa ofisini tu bali ni
kuhakikisha tunawajengea mahusiano mema na kutatua matatizo kwa wale
tunaowaongoza, ni ushindi kwa Taff leo hii Jack na Tico wanapatanishwa
na kuwa kitu kimoja,”anasema Mwakifwamba.
Bongo Movies.Com inawapongeza wote waliofanikisha kulimaliza hili na kuwatakia kila la kheri wakali hao kwenye kazi zao.
Post a Comment