Katibu Mkuu Uvccm Taifa Sixtus Mapunda akivalishwa skafu na kiongozi wa green Gard mara baada ya kuwasili katika Ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya April 25 mwaka huu. |
Vijana wakiwa makini kufuatilia yanayoendelea katika mkutano huo. |
Katibu Mkuu Uvccm Taifa Sixtus Mapunda akizungumza katika Mkutano huo |
Na Emanuel Madafa,Mbeya
KATIBU
Mkuu wa Vijana CCM Taifa, Sixtus Mapunda, ameitaka kamati ya siasa ya chama cha mapinduzi ccm Mkoa wa
Mbeya kuacha kukivuruga chama kwa maslahi yao binfasi hususani katika kipindi
hiki cha kuelekea katika uchaguzi Mkuu mwezi Octoba..
Amesema
mpasuko uliopo ndani ya chama hicho hususani kwa Jumuiya hiyo ya Uvccm , Mkoa
wa Mbeya, unatokana na makundi ya wajumbe wa kamati za siasa ambao ndani yao
wamo wabunge, wanaotaka nafasi ya ubunge na udiwani na nafasi nyingine za ngazi
ya juu .
Akizungumza
na vijana wa CCM Wilaya ya Mbeya katika ukumbi wa mikutano wa ccm , Mapunda
amesema, mipasuko hiyo inatokana na baadhi ya wajumbe hao wa kamati za siasa
kuwa na uchu wa kuwania madaraka, hali
ambayo imechangia kwa kiasi kikubwa kukivuruga chama .
Aidha, amesema uvccm
haitainyamazia hali hiyo, wala kuona kamati hizo za siasa zikikivuruga chama
kupitia vijana badala yake kitashughulika na hao wachache kwa kutengeneza
mikakati ya kuwakuwango'a
Amesema
jumuiya hiyo haitakubali kuona mivutano yao ya kisiasa inakivuruga chama vinginevyo wachague moja kubaki ndani ya kamati hizo kama wajumbe
au kuondoka mapema bila kushurutishwa.
Amesema
wajumbe wa kamati ya siasa wanaotaka ubunge waachane na kamati ya siasa
wakagombee nafasi kwani chama kina agenda ya kurudisha jimbo na kuleta heshima
ya chama hivyo hawatavumilia kuliona hilo likiendelea.
Amesema,
UVCCM Taifa, haikubaliani na ‘Upuuzi huu’ na hawako tayari kuona mivutano
ikiendelea ndani ya chama inayosababishwa au kuchangiwa na wajumbe wa kamati za
siasa na kwamba tunatoa angalizo kwa wahusika hao kuchagua moja, kama wanataka
kuwaongoza au kuendelea na harakati zao za siasa.
Amesema,
haiwezekani viongozi ambao wanategemewa kukiweka chama sehemu nzuri, mkawaweka
vijana njiapanda, huku wakifahamu fika vijana ndio tegemezi kwa chama na Taifa.
Hata hivyo amewataka vijana hao
kuhakikisha wanaweka nguvu ya pamoja katika kuhakikisha wanalikomboa jimbo hilo
la mbeya mjini linalotawaliwa na Upinzani .
Amesema hadhi ya wanambeya imeshuka
kwa kiwango kikubwa kutokana na jimbo kuongozwa na mtu asiye na uwezo hivyo
mkakati uliopo sasa ni kulikomboa jimbo hilo bila kujali ni nani atasimamishwa
na chama cha Mapinduzi.
Katika hatua nyingine Katibu Mkuu
huyo amewataka watumishi wa serikali wanaokwamisha juhud za serikali katika kuleta
maendeleo kwa wananchi kuchukua tahadhari mapema vinginevyo chama
kitawachukulia hatua kali za kinidhamu badala yake watambue kuwa wapo katika nafasi hizo kwa kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi ambacho ndicho chama tawala.
Mwisho.
Post a Comment