| Meya wa jiji la Mbeya Atanas Kapunga. |
Kufuatia kauli ya Mbunge wa jimbo la mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (Sugu )kudai kuwa meya wa jiji hilo Atanasi Kapunga kuwa ametengeneza
mikakati ya kuligawa jimbo la mbeya kwa maslahi yake binafsi nakwamba sababu
zilizotolewa na meya huyo ni za kibabaishaji .
Akizungumza mjini Dodoma hii leo mbunge huyo amesema sababu za kibabaishaji za meya huyo juu ya wa ugawaji wa jimbo la mbeya mjini kwani ni sawa na kugawa moyo wake,
Kutokana na kauli hiyo msahiki
meya wa Jiji la Mbeya, Athanas Kapunga, ameibuka
na kudai kuwa hana sababu ya
kuendelea kujibidhana na Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini Joseph Mbilinyi
kwani amekuwa akimpa changamoto za kiutendaji ambazo zimemfanya kufanikiwa
katika ufanisi wake wa kazi.
Amesema, Mbunge huyo anapaswa kusubili Tume ya uchaguzi itakapotoa
kibali cha kuingia ulingoni kuliko kuendelea kulitumia Bunge kama sehemu ya
kuwachafua watu ambao hawana nguvu ya kisheria ya kujibu tuhuma hizo Bungeni.
Akizungumza na blog hii Kapunga amesema
, Sugu ni
mjumbe wa vikao vya kiutendaji vya halmashauri ananafasi kubwa ya kufika na
kuyazungumzia hayo tatizo linalomsumbua ni upeo wake mdogo wa kufikiri hivyo
kujiaminisha kwamba Jimbo la Mbeya ni mali yake.
Alisema,Jimbo
hilo ni la wananchi, si la ukoo na kitendo cha kuwaza jimbo ni mali yake ni
ujinga, yeye atabaki kuwa kwenye horodha ya wabunge wa ajaabu ambao kila
siku kazi yake ni kumuwaza Kapunga badala ya kusimama na hoja.
Amesema, wakazi wa Mkoa wa Mbeya ni watu ambao wameelimika hivyo
hawapendi kudanganywa ni watu wanaojipenda na niwachapakazi hivyo majungu ya
watu wachache hayawakatishi tama zaidi ni kufanya kazi.
Alisema, wananchi wanachotaka wao ni kiongozi bora na si kiongozi
mbabaishaji , kiongozi anayetoa miongozo yenye maendeleo na misimamo.
Hata hivyo Kapunga alitumia
nafasi hiyo kutoa ufafanuzi kuhusu hali halisi ya utendaji kazi wake uliokuwa
umezungukwa na majungu, chuki na fitina zisizokuwa na msingi zinazoendelea
kutolewa na Mbunge Sugu aliyemfananisha na chipukizi wa kisiasa.
Amesema, majungu,fitina na chuki zilizokuwa zinatawala juu yake
zimekuwa zikimsaidia kufanya kazi kwa bidii ili wale wote wanaoeneza ujinga
akiwemo Sugu, waje kuonekana ni wapumbavu.
Amesema, mchakato wa kuligawa jimbo hilo, ulianza mwaka 2008 ukiwa
chini ya Mbunge Mpesya hivyo yeye kama Meya ni jukumu lake kulisemeya
hilo kama mtendaji wa halmashauri.
Mwisho.






Post a Comment