Timu
ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) jana imepoteza mchezo wa pili
mfululizo katika michuano ya kombe la Cosafa, baada ya kufungwa mabao 2 -
0 na Madagascar, mchezo uliofanyika katika uwanja wa Royal Bafokeng
jijini Rustenburg.
Kwa
Taifa Stars kupoteza mchezo huo, moja kwa moja inakua imeaga michuano
katika hatua ya makundi, kutokana na kubakisha mchezo mmoja tu wa
kukamilisha ratiba dhidi ya Lesotho utakaochezwa kesho ijumaa katika
uwanja wa Moruleng.
Katika
mchezo huo wa jana, Taifa Stars ilishindwa kuonyesha makali yake mbele
ya timu ya Madagascar na kupelekea kufungwa mabao 2 katika dakika 45 za
kipindi cha kwanza.
Sehemu
ya ushambuliaji ya Taifa Stars haikua na madhara yoyote langoni mwa
Madagascar, huku sehemu ya ulinzi iLijikuta na wakati mgumu muda wote
kuzuia hatara za washambuliaji wa Madagascar.
Mara
baada ya mchezo huo, kocha wa Stars Mart Noij alisema amesikitishwa na
matokeo hayo, kwamba hakutegemea kupoteza mchezo dhidi ya Madagascar.
“Timu
yangu haikucheza vizuri, haikuweza kutengeneza nafasi nyingi za kufunga
, huku wapinzani awetu wakitumia nafasi mbili walizozipata kupata mabao
mawili katia mchezo huo” alisema Nooij.
Mpaka
sasa kundi B la linaongozwa na Madagscar yenye ponti 6 sawa na
Swaziland yenye pointi 6 pia zikiwa na tofauti ya magoli ya kufunga na
kufungwa, na mchezo wa mwisho utakaowakutanisha kesho ndio utakaoamua
nani atatinga hatua ya robo fainali.
Kufuatia
Taifa Stars kupoteza michezo yote miwili, inaungana na Lesotho kutoka
kundi B kuaga michuano hiyo, huku kundi A timu za Mauritius na
Shelisheli zikiwa zimeshaaga michuano hiyo pia.
Stars
inatarajiwa kurejea nyumbani Tanzania kesho iumaa usiku mara baada ya
mchezo wake wa mwisho dhidi ya Lesotho utakochezwa kesho jioni.






Post a Comment