Shughuli ya upigaji kura inaendelea nchini Uingereza katika uchaguzi mkuu.
Mamilioni ya watu wanashiriki uchaguzi huo baada ya wiki tatu za kampeni kali.
Wagombea wa vyama vikuu vya kisiasa walijitokeza mapema kupiga kura zao .
Uundwaji wa serikali ijayo utategemea chama ama muungano utakaokuwa na wajumbe wengi bungeni .
Tume
ya uchaguzi nchini Humo imesema kuwa inatambua malalamishi kwamba
waingereza wachache wanaoishi nchi za kigeni hawakupokea makasha ya
karatasi za kupigia kura yaliyotumwa kwao kwa njia ya posta katika muda
wa kupiga kura .
Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa mapema leo nchini Uingereza ambapo takriban
watu milioni 50 wamesajiliwa kama wapiga kura.
Jumla ya wabunge 650 watachaguliwa kote nchini Uingereza.
Vituo vya kupigia kura karibu 50,000 nchini kote vilifunguliwa saa moja asubuhi kwa saa za Uingereza.
Jumla ya wabunge 650 watachaguliwa kuingia bunge la nchi hiyo, kukiwa na watu karibu milioni 50 waliojiandikisha kupiga kura.
Kama ilivyo kwa uchaguzi mkuu, kuna viti zaidi ya 9,000 vya madiwani vinavyogombewa katika serikali za mitaa 279.
Mameya pia watachaguliwa katika miji ya Bedford, Copeland, Leicester, Mansfield, Middlesbrough na Torbay.
Hii ina maana kuwa karibu kila mpiga kura wa England, ukiondolewa mji
wa London ambako hakuna uchaguzi wa serikali za mitaa, atapewa karatasi
mbili za kupigia kura watakapofika katika kituo cha uchaguzi.
Baadhi
ya kura tayari zimekwishapigwa kupitia vituo vilivyoko nje ya Uingereza
kwa kutuma kura kwa njia ya posta. Kura hizi zilikuwa ni asilimia 15%
ya kura zilizopigwa katika uchaguzi mkuu wa 2010 wakati watu
waliojitokeza walikuwa asilimia 65%.
Masanduku ya kupigia kura yamepelekwa katika vituo vya uchaguzi.
Kwa mara ya kwanza, watu waliweza kujiandikisha kupiga kura kupitia njia ya mtandao.
Vituo vingi vya kupigia kura
viko katika majengo ya shule, kumbi za vituo vya kijamii na kwenye kumbi
za parokia, lakini migahawa, maeneo ya kufua na kunyosha nguo na basi
la shule pia vitatumika kama vituo vya kupigia kura.
Vituo vya
kupigia kura vitafungwa saa nne usiku kwa saa za Uingereza, lakini
maafisa wa uchaguzi wamesema mtu yeyote ambaye atakuwa kwenye mstari
kufikia wakati huo ataweza kupiga kura yake.
BBC itatangaza moja kwa moja kuanzia saa tatu na dakika 55 usiku shughuli za uchaguzi katika kaunti 220.
Matangazo
kamili kuhusu matokeo yanavyopokelewa yatakuwa katika ukurasa wa
mtandao wa BBC politics online live na katika sehemu ya mbele ya ukurasa
wa uchaguzi, ikiwa ni pamoja na taarifa zote mpya kutoka sehemu
mbalimbali nchini na uchambuzi wa waandishi wa habari.
Vituo vingi vya kupigia kura viko katika majengo ya shule, kumbi za
vituo vya kijamii na kwenye kumbi za parokia, lakini migahawa, maeneo ya
kufua na kunyosha nguo na basi la shule pia vitatumika kama vituo vya
kupigia kura.
Vituo vya kupigia kura vitafungwa saa nne usiku kwa
saa za Uingereza, lakini maafisa wa uchaguzi wamesema mtu yeyote ambaye
atakuwa kwenye mstari kufikia wakati huo ataweza kupiga kura yake.
BBC itatangaza moja kwa moja kuanzia saa tatu na dakika 55 usiku shughuli za uchaguzi katika kaunti 220.
Matangazo
kamili kuhusu matokeo yanavyopokelewa yatakuwa katika ukurasa wa
mtandao wa BBC politics online live na katika sehemu ya mbele ya ukurasa
wa uchaguzi, ikiwa ni pamoja na taarifa zote mpya kutoka sehemu
mbalimbali nchini na uchambuzi wa waandishi wa habari.
Post a Comment