Na Baraka Kizuguto,Dar es salaam
Kocha
Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Mart Nooij leo
ametangaza kikosi cha wachezaji 28 watakaoingia kambini katika hoteli ya
Tansoma iliyo eneo la Gerezani jijini Dar es salaam, kujiandaa na
michuano ya kombe la COSAFA na kuwania kufuzu kwa AFCON na CHAN mwezi
Juni mwaka huu.
Akiongea
na waandishi wa habari leo makao makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu
nchini TFF amesema, wachezaji 28 aliowaita, amewaona kwa macho yake
wakicheza, na katika wachezaji aliowaita amechanganya wanaochipukia
(damu changa) na wenye uzoefu wa michuano ya kimataifa.
Nooij
amesema katika orodha hiyo ya wachezaji 28 watakaoripoti kambini
jumatatu mchana, watapimwa afya zao na madakatari wa timu ya Taifa, na
kisha watakaokuwa fit atachagua wachezaji 20 watakaokwenda kwenye
michuano ya COSAFA nchini Afrika kusini.
Aidha
Nooij ameongeza wachezaji 8 watakaobakia nchini wanapaswa kuwa tayari
wakati wowote wanaweza jumuishwa katika kikosi kutokana na Taifa Stars
kukabiliwa na michuano mbalimbali ambayo pia inahitaji kuwa na wigo
mpana wa wachezaji.
Wachezaji
walioitwa na kocha Nooij ni magolikipa: Deogratius Munish (Yanga),
Aishi Manula, Mwadini Ali (Azam), walinzi: Shomari Kapombe, Aggrey
Morris, Erasto Nyoni (Azam), Nadir Haroub, Oscar Joshua, Kelvin Yondani
(Yanga), Abdi Banda, Hassan Isihaka (Simba), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar)
na Haji Mwinyi (KMKM).
Wengine
ni viungo: Amri Kiemba, Salum Abubakar, Frank Domayo (Azam), Said Juma,
Salum Telela, Hassan Dilunga (Yanga), Said Ndemla (Simba), Haroun
Chanongo (Stand United) na Mwinyi Kazimoto (Al Markhira).
Washambuliaji
ni Ibrahim Ajib (Simba), Mrisho Ngasa, Saimon Msuva (Yanga), John
Bocco, Kelvin Friday (Azam) na Juma Luizio (Zeco United).
Taifa
Stars inatarajiwa kuondoka nchini siku ya jumatano, Mei 13 saa 1 jioni
kwa shirika la ndege la Fastjet kuelekea nchini Afrika Kusini katika mji
wa Rusterburg - North West Province ambapo ndipo michuano ya COSAFA CUP
itafanyika kuanzia Mei 17 mpaka Mei 31 mwaka huu.
Mchezo
wa kwanza wa Taifa Stars iliyopo katika kundi B katika michuano ya
COSAFA, itacheza dhidi ya Swaziland Mei 18, Mei 20 (Madagascar Vs
Tanzania) na Mei 22 ( Tanzania vs Lesotho), mshindi wa kundi B atacheza
robo fainali dhidi ya timu ya Taifa kutoka Ghana.
Mara
baada ya kumalizika kwa michuano hiyo, Taifa Stars itarejea nchini
kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu kwa AFCON 2017, dhidi ya Misri
utakaopigwa Juni 13 nchini Misri, kisha kurejea nchini kucheza na Uganda
Juni 21 kuwania kufuzu kwa fainali za wachezaji wa ndani CHAN.
Mart Nooj amesema ataitumia michuano ya COSAFA kama sehemu ya maandalizi ya michezo ya kuwania kufuzu kwa AFCON na CHAN.
Mwisho.
Post a Comment