|
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi CCM (UVCCM) Mkoa wa mbeya , Amani Kajuna, akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi katika
eneo la sogea Tunduma wilayani mombaMei 4 mwaka huu. |
|
Wanachama wa ccm na wananchi wakimsikiliza Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Uvccm Mkoa wa mbeya Amani Kajuna katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Sogea Tunduma Wilayani Momba. |
|
Mwenyekiti Kajuna akizungumza na wananchi na wanachama wa ccm katika mkutano huo uliofanyika katika eneo la Sogea Tunduma Momba Mkoani Mbeya Mei 4 mwaka huu. |
|
Mjumbe wa kamati ya siasa Mkoa Hasani Nyalile akizungumza katika mkutano huo.
|
|
Katibu wa Uvccm Mkoa wa Mbeya Adia Mamu akizungumza na wanachama wa ccm na wananchi walifika katika mkutano huo eneo la sogea Tunduma Momba Mkoani Mbeya Mei 4 mwaka huu.
|
|
Msanii wa Nyimbo za Asili Awilo akitumbuiza katika mkutano huo. |
|
Mkutano ukiendelea |
|
Kikundi cha sanaa cha Makirikiri kikitoa burudani katika Mkutano huo ulioandaliwa na Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Mbeya chini ya Mwenyekiti Amani Kajuna Mei4 mwaka huu.Picha Emanuel Madafa |
Umoja wa vijana wa ccm mkoa wa mbeya(uvccm)
umetoa siku tatu kwa mbunge wa jimbo la momba david sillinde kuziwasilisha
fedha za mfuko wa ujimbo kiasi cha shilingi milioni 46 anazodaiwa kuzihafadhi
kwa ajili ya kumsaidia kwenye kampeni yake ili zifanyie maendeleo
Akizungumzia hilo, mwenyekiti wa umoja huo,
amani kajuna, katika mkutano wa wananchi katika eneo la sogea tunduma wilayani
momba, amesema sillinde anapaswa kuziwasilisha fedha hizo kwenye mamlaka husika
ili zifanyie shughuli za maendeleo.
''Kiasi hiki cha fedha cha shilingi milioni
46 kinatokana na kodi za wananchi na ni kwa ajili ya kutekeleza shughuli za
maendeleo hivyo kitendo cha mbunge kuzikumbatia ni ukiukwaji wa sheria, umoja
wa vijana tunamtaka kuziwasilisha fedha hizo ndani ya siku tatu,"
Aidha, mwenyekiti huyo, amechangia mifuko 10
ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa kisima cha maji katika eneo la sogea mjini
tunduma.
Mwisho.
Post a Comment