Na Mwandishi Wetu, Singida
MDAI katika Kesi ya madai ya talaka Magreth Mwangu dhidi ya Mkurugenzi wa Shule ya St. Mathew, Thadei Mtembei amehoji uhalali wa mahakama kufikia kukagua mali zake siku ya Jumamosi bila kupitia mahakama yoyote hapa Singida.
Kesi hiyo ambayo inasikilizwa mahakama ya Mwanzo Kizuiani Mbagala Jijini Dar es Salaam, juzi (Jumamosi) ililazimika kuhamia mkoani Singida baada ya mdaiwa (Thadei Mtembei) kuitaka mahakama kuhamia mkoani Singida kwa gharama zake ili kuhakiki nyumba ambazo alidai alimjengea Mwangu.
Mtembei katika hoja yake ya kuitaka mahakama kuhamia Singida alisema yuko tayari kulipa gharama zote ikiwemo nauli na posho.
Hakimu anayesikiliza kesi hiyo Rajab Tamaambele, na wakili wa Mtembei ambaye ni mtoto wa mke mkubwa wa Mtembei (Peter Mtembei), karani na kesi na mtumishi wa mahakama ni miongoni mwa watu waliofika kwa ajili ya ukaguzi na uhakiki wa nyumba hizo.
Hata hivyo hakukuwepo na wazee wa baraza jmbo ambalo mwangu pia alililalamikia. Mwangu alidai kuwa licha ya kuwa hafahamu sheria kutokana na kutokuwa na elimu hata ya Sekondari lakini kitendo cha mahakama kufika Jumamosi kwa ajili ya kufanya uhakiki na ukaguzi haioni kama ni ha haki na pia kulikuwa hakuna afisa ustawi wa jamii.
Alidai hakimu kuongozana na wakili wa kesi hiyo na kuwa pamoja muda wote haoni kama atatendewa haki katika shauri hilo.
“Mimi nahoji ushirikiano huu kama utanitendea haki kwani watu wametoka pamoja Dar es Salaam wameongozana kwenye magari binafsi nafika eneo la tukio nakuta msafara wa hakimu, wakili wa mdaiwa, mwenyekiti wa kitongoji ukiwa umeshafika mbele ya nyumba ambayo walitaka kuanza kuihakiki” alidai.
Alidai hata Mwenyekiti wa Mtaa wa Sabasaba, Mahamoud alisema hajapewa taarifa yoyote ya maandishi kwani alishtukizwa na kupelekwa kwenye nyumba hiyo ambayo alisema hafahamu kama ni ya Mwangu.
Pia alihoji uhalali wa mtoto wa Mtembei ambaye ni wakili kusimamia shauri hilo katika mahakama ya Mwanzo huku mara kadhaa akimtolea maneno ya kashfa kama ni mfunga vidonda tu hawezi kujenga nyumba.
Mwangu alisema alishawahi kuiambia mahakama kuwa nyumba zake za Singida alizijenga na aliamua kuziuza kwa ajili ya elimu ya watoto wake ambao walitelekezwa na baba yao lakini cha kushangaza mahakama kwa amri ya Mtembei ikataka kufika Singida kuhakiki nyumba zake.
Hata hivyo mahakama ilikagua nyumba tatu ambapo moja ilikuwa imeshauzwa kwa Sh. Milioni 15 na nyingine iliuzwa ikiwa katika hatua ya msingi.
Baada ya kumalizika kwa uhakiki huo hakimu Tamaambele alimtaka Mwangu kuhakikisha anawasilisha mahakamani nyaraka zote za nyumba na kuwapeleka watoto mahakamani kabla ya kesi hiyo kutolewa hukumu Agosti 25, mwaka huu.
Post a Comment