Na Mwandishi wetu,Mbeya
BAADHI ya wananchi wa Mkoa wa Mbeya, wamekitaka chama cha
mapinduzi, kutoa onyo kali kwa wanachama wake ambao ni miongoni mwa wagombea
nafasi ya ubunge Jimbo la Mbeya mjini, kuacha kutoa matamshi yanayoashiria
vitendo vya ubaguzi wa kikabila.
Wakizungumza jiji Mbeya , mara baada ya chama hicho
kupitia wilaya kutangaza matokeo ya uchaguzi wa ubunge kwa wagombea 16 ambao walijitokeza kuwania nafasi
hiyo.
Walisema, chama kama chama hakijaundwa wala kuongozwa na sera
ya ubaguzi wa aina yoyote ile hivyo wanashangazwa na matamshi ya ubaguzi
yanayotolewa na baadhi ya wagombea hao.
“Hivi leo chama kimefikia hatua ya kuwakumbatia watu
ambao wanaeneza sera ya ukabila hii ni hatari kwa Taifa letu kwani ni uchochezi
na ukiachwa utaliangamiza taifa hili,”alisema God Julius mkazi wa majengo
ambaye pia ni mwanachama wa chama cha mapinduzi.
Alisema, kunahatari ya kukipoteza chama kwa makosa madogo
ambayo yamekuwa yakifumbiwa macho na viongozi na wakati mwingine kufanywa na
viongozi hao.
“Leo mwanachama wa ccm anasimama na kusema jimbo haliwezi
kuongozwa na mtu ambaye si mzawa na kumfafanisha mtu huyo sawa na kibaka, hilo
ni tendo la aibu na si uungwana wakati
umefika kwa chama kuchukua hatua,”alisema.
Alisema, CCM ni sawa na taasisi kwani imeundwa kwa
kufuata miongozo na kuongozwa kwa taratibu na sheria na ikumbukwe kwamba chama
kimebaba watu tofauti tofauti na makabila tofauti hivyo watu wakianza kubaguana
kwa ukabila ni ishara mbaya ambayo inaweza sababisha vita vya wenyewe kwa
wenyewe.
“Katiba na sera ya CCM inaeleza kwamba kila mtu mbaye ni
mtanzania anahaki ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya chama hivyo,
tukianza kubaguana hii ni hatari,”alisema Mwajabu jamari mkazi wa Soweto.
Alisema, wagombea wanasimama kwenye umati wa watu na
kushangilia huku wakitoa kauli za chuki kwa wagombea ambao si wazawa ni vema chama
kikachukua hatua za kinidhamu.
Hata hivyo, aliwatahadharisha wagombea hao kwamba
wakumbuke familia zao zinaishi kwenye mikoa mbalimbali hivyo na wao
wakibaguliwa wasishangae.
Mwisho.
Mwisho.
Post a Comment