Bibi kizee mmoja mwenye umri wa
miaka 85 raia wa Marekani na ambaye amekuwa akiiba vito vya thamani kwa
zaidi ya miaka 60 amehukumiwa tena kwa kosa la wizi.
Doris Payne,
anatuhumiwa kwa wizi wa herini ya thamani ya dola 690, kutoka katika
duka moja la uuzaji wa vitu vya thamani la Saks katika kiunga kimoja
mjini Atlanta-Marekani.Wakili wake anatafuta namna ataachiwa huru kwa sababu ya kudorora kwa afya yake.
Payne, ambaye maisha yake ya wizi yaliwekwa katika filamu mwaka 2013, amewahi kufungwa jela mara kadhaa kwa makosa mengi tu ya wizi na uhalifu.
Wakuu nchini Marekani wanasema kuwa, ametumia majina 22 ya bandia tangu alipoiba almasi kwa mara ya kwanza akiwa na umri wa miaka 23, na akaweza kukwepa kutiwa mbaroni.
Muungano wa Walinzi wa vitu vya thamani JSA, kampuni moja kubwa ya kibiashara, ilituma tahadhari kwa maduka yote yanayouza bidhaa na mapambo ya thamani kujihadhari na mwizi huyo sugu mapema miaka ya 70.
Rais wa kampuni hiyo kubwa alitaja tabia ya bi kizee huyo kama wizi au uhalifu wa aina yake.
Aidha anastaajabu kuwa angali anaiiba hata akiwa na umri huo mkubwa.
Akihojiwa na shirika la habari la Associated Press mwaka 2005, akiwa jela, bibi huyo Payne, alisema kuwa haibi kwa sababu ya pesa; ila yeye hujikuta tu akiiba na haoni kama ataacha tabia hiyo, labda baada ya kufa.CHANZO BBC
Post a Comment