Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi.
Na Mwandishi wetu,Mbeya,Jamiimojablog
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwanaume mmoja Mkazi
wa kijiji cha Malolo Ndugu Chipunguli Mkisi
(30) amemuua mke wake kwa kumkata panga kichwani kisha yeye mwenyewe kujiua kwa kujinyonga.
Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Mbeya Ndugu Ahmed Msangi amesema tukio hilo la aina yake limetokea Desemba 15
mwaka huu majira ya saa 7 mchana huko katika kijiji cha Malolo, Kata ya Msia,
wilaya ya Mbozi, Mkoa wa Mbeya.
Msangi amemtaja mwanamke huyo kuwa ni Neva Mwaweza (24) Mkazi wa Malolo ambaye ameuwawa na mumewe kwa kukatwa panga kichwani .
Kamanda Msangi amesema chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi baada ya mwanaume
kumtuhumu mke wake kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine.
inadaiwa kuwa baada ya tukio, mtuhumiwa alijinyonga
kwa kutumia kamba kwenye mti umbali wa mita 100 kutoka nyumbani kwake.
Aidha mwili wa marehemu [mwanaume] ulikutwa ukiwa na
majeraha kwenye vidole na kando kukiwa na panga na alikutwa na ujumbe uliokuwa
na maneno “kuwa ameamua kumuua mke wake
na yeye kujinyonga kutokana na mke wake kuwa na mahusiana ya kimapenzi na
mwanaume mwingine aitwae kilasi nzowa”
Miili ya marehemu
imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya vwawa. ambapo kwa mujibu Kamanda Msangi
uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.
Mwisho.
|
Post a Comment