Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Na DKT BOAZ MKUMBO MD
Napenda niseme kwamba watu wengi tuna shauku sana na hamu sana yakuishi bila kitambi na bila uzito mkubwa ambao wengi umetulemea.
Wengi wetu tumekuwa tukirusha lawama mbalimbali kwamba uzito ni ugonjwa wakurithi. Sio kweli kwa herufi kubwa.

Moja ya tafiti iliyofanywa na Dr Collin Campbell ambaye ni profesa aliyebobea kwenye lishe ya mimea na mfanya tafiti maarufu. Alichukua mapacha wawili wanaofanana na wanao ishi katika mazingira tofauti akawafanyia tafiti kwa kuwafuatilia wanaishi maisha gani? Tafiti hii ilifanyika Retrospective.
Baada ya miaka kadhaa, alikuja kugundua kuwa yule mtoto aliyekuwa anapewa vyakula vyenye wanga nyingi, vyenye sukari nyingi aliishia kupata uzito mkubwa na kupata kisukari cha utotoni yaani type 1 Diabetes. Yule pacha mwingine aliishi maisha ya uzito wenye afya na bila kitambi kwa sababu alikuwa anakula vyakula kama mboga za majani, vyakula vya kujenga mwili na aliepuka kabisa ulaji wa wanga nyingi na vyakula vya sukari nyingi.

Hio tafiti inaonesha kwamba, wote hapa tuna genes au vina saba za urithi za magonjwa sugu kutoka kwa wazazi. Lakini endapo ukiishi maisha ya kutouvuruga mwili kuitendaji basi hutayaibua magonjwa hayo.
Kwa hio hata mimi hapa nina chembechembe za uzito uliokithiri ni jukumu langu kuzichokoza ili zibadili mtazamo na uzito uanze kuongezeka bila sababu. Hio ndio sababu kuwa unakuta mwingine ana uzito wa kawaida lakini mwingine uzito mkubwa na kitambi juu.

Hivyo njia pekee ni kuepuka ulaji wa vyakula vinavyobadili mtazamo wa utendaji wa mwili wako na hapo ndipo utaishi bila ugonjwa wowote kabisa.
DIETING, Imekuwa changamoto kwa wengi utasikia maelezo haya
‪#‎Unakula‬ sana Punguza ulaji !
‪#‎Hufanyi‬ mazoezi jitahidi sana
#Unakula Ugali wa sembe acha kula dona
#Unakula mchele mweupe
‪#‎Epuka‬ mikate mweupe
Utaambiwa kila imani na unafanya chochote lakini unashangaa uzito unaendelea kupanda kila siku.

Mazoezi ni kwa watu wanao imarisha miili yao na sio kwa kupunguza tumbo na uzito mkubwa, Siri kubwa ni KUBADILI MLO WAKO KATIKA SAHANI YAKO. Tiba ya KITAMBI NI JIKONI SIO GYM.
SHERIA ZA KUPUNGUZA UZITO KATIKA PROGRAM YANGU.
1.Punguza kula vyakula vyenye wanga nyingi katika chakula chako na punguza kabisa ulaji wa vyakula vyenye sukari nyingi.
Mfano:
Mikate
Tambi
Ugali
Wali
Matunda juisi
Viazi vitamu
Viazi mviringo
Miwa
Mihogo
Vyakula na vinywaji vya viwandani.

2. Kula vyakula asilia tu, sio vyakula vilivyowekewa kemikali za kudanganya ulimi wako kuwa ni tunda kumbe sio kweli.
3. Epuka Udanganyifu katika Mlo huu
4. Kula vyakula vyenye mafuta mengi, protini kidogo na mboga za majani aina zote.

Protini ni km
-Nyama ya ng'ombe,mbuzi,kondoo, swala, kuku, bata, samaki aina zote, karanga, Flaxseed. Nk

Fats
Mayai, nyama ya mafuta ,olive oil, Alizeti,coconut nk
Mboga za majani
Spinach
Kabeji
Sukuma wiki
Cauli flower
Broccoli
Nk

5. Kula kwa sababu una njaa tu na sio kwa sababu saa sita imefika . Usitumie ratiba hakkikisha unakula pale unapokuwa una njaa pekee tu.
6. NI MARUFUKU KUJINYIMA, HAKIKISHA UNAKULA UNASHIBA LAKINI USIVUKE MIPAKA KWENYE SHERIA ZETU. Huruhusiwi kula kiugali kidogo, wali kidogo km ishara ya kupunguza wanga, bali ongeza protini katika mlo wako na mafuta utafurahia unavyopungua uzito.
Hizo ni baadhi ya sheria sita ukizingatia afya yako itakuwa yakipekee kabisa.
Asante.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top