Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
-Hutengeneza ukuta wa seli za binadamu.
-Hutengeneza homoni za mwilini mwako hasa za zinazo husika na uzazi kwa mwanamke na mwanaume.
-Hutengeneza nyongo ambayo husaidia mfumo wa mmeng'enyo wa chakula kumeng'enya chakula ipasavyo.
Ndio maana napenda siku zote kusema kuwa wanaokwambia Fat ni mbaya wanakupotosha, wanakwambia cholesteral ni mbaya wanakupotosha hata mwalimu wangu wa biochemistry aliniambia hili alijua jinsi gani jamii tunachukua taarifa juu juu na kuzibeba bila kujali utapungukiwa nini hasa endapo ukkiepuka kwa muda mrefu.
NASEMA
NO CHOLESTERAL NO LIFE EXISTANCE, FACT!
Dondoo za afya kama unahitaji kupunguza uzito.
1. Hii ni molekyuli ndogo kabisa inayopatikana mwilini mwako ambayo
-Mwili inatengeneza
-Mwili unahifadhi
-Mwili unaitoa nje kama taka mwili.
2. Wingi wa cholestero mwilini mwako na kazi zake hii ina maanisha kuwa.
KAMA HAKUNA CHOLESTERO MWILINI =HAKUNA UHAI
i.e No cholesteral =No life.
3. Kuna mifumo miwili ya cholestero mwilini mwako,
-Cholestero huru [Unesterified cholesteral]
-Cholestero Isiyo huru [Esterified cholesteral]
Mifumo hio miwili ndio inayokupa uwezekano wa kuweza kuhifadhiwa au hapana.
4. Cholestero nyingi tunayokula kwenye chakula ni cholestero ambayo haiwezi kufyonzwa na mwili na kuingia katika mwili wako na hatimaye kuongeza kiwango cha cholesteral kwenye damu.
Mwili wako, hutengeneza cholestero huru na kuifadhi kwenye ini na hii ndio huzuia kuchukuliwa kwa cholesteral ambayo inatokana na mlo wako kwani ni cholesteral ambayo sio huru na hushindana na cholesteral huru inayotengenezwa na ini lako.
Asilimia kubwa ya cholesteral ambazo ni msingi mkubwa ktk mwili hutengenezwa na mwili wenyewe na asilimia chache sana hupatikana kupitia lishe tunayokula. Na cholestero inayotengenezwa na mwili wako ndio chanzo msingi cha mwili wako kuweza kuishi.
-Mwili unatengeneza cholestero ambazo ni huru ambazo zinazuia kufyonzwa kwa cholesteral kutoka katika lishe katika utumbo mwembamba.
-Na cholestero inayotokana na vyakula asilimia kubwa [karibia] yote hutolewa nje kwa njia ya kinyesi.
Ndio maana nilisema, Tunatengeneza cholestero,Tunahifadhi cholestero,Na tunaitoa cholestero kama taka mwili.
Note: Ulaji wa vyakula vyenye Cholesterol zina uwezo mdogo sana wa kuongeza kiwango cha cholesteral mwilini mwako, maana cholestero inayotokana na lishe ni [Esterified au siyo huru] hivyo hutolewa yote nje kwa njia ya haja kubwa.
5. Cholesterol husafilishwa kutoka kwenye ini na kwenye Utumbo mwembamba kwa kutumia vitu vikuu viwili.
-HDL [High density lipoprotein]
Hivi ni visafirisha cholestero kutoka kwenye mishipa ya damu na kuimarisha mishipa ya damu.
Tunahitaji kiwango kingi sana cha HDL ili tusiweze kupata magonjwa ya moyo.
-LDL [Low density Lipoprotein]
Hizi ni molekyuli pia ambazo zinapeleka cholesteral kwenye mishipa ya damu.
Miili yetu inahitaji kiwango kidogo cha LDL ili kuepuka magonjwa tabia.
Kwa nini Cholesteral haisafirishwi na damu ? Ina usafiri wake maalumu kama HDL na LDL?
Hii ni kwa sababu cholesteral haiambatani na maji kwani asilimia kubwa ya damu ni plasma na kiwango kikubwa cha plasma ni maji.
Kwa kitaalamu tunaweza kusema cholestero ni HYDROPHOBIC
Hydro= Maji
Phobic= Enye kuogopa.
Ndio maana basi kwenye damu kukawepo na visafirisha cholestero maalumu ambavyo ni LDL na HDL.
JE VYAKULA VYA MAFUTA VINAONGEZA CHOLESTERAL KWENYE DAMU?
Tafiti zinaonesha kwamba vyakula vyenye mafuta vina uwezo mdogo sana wa kuongeza kiwango cha cholesteral mwilini kwa sababu nilizo eleza hapo juu.
Na ndio maana nchi kama Canada wakatengeneza Nutrional Guideline [Mwongozo wa lishe yenye kuruhusu vyakula hivi vitumike bila woga]
JE VYAKULA VYA WANGA VINAONESHA TAFITI GANI KATIKA KUPUNGUZA UZITO NA KUONGEZA KIWANGO CHA HDL NA LDL.
Vyakula vya wanga kwa wingi vinaonesha kusababisha uzito mkubwa kupita kiasi,kupunguza kiwango cha HDL ambacho ni msaada kwetu kutoa au kusafisha cholesteral kwenye mishipa.
Na ukweli utabaki pale pale kuwa vyakula hivi ndio visababishi vikubwa vya uzito kupita kiasi.
TAFAKALI KWA LEO.
Kama unaogopa ulaji wa vyakula vya mafuta kama Karanga, Siagi ya karanga [peanutbutter], Alizeti,Olive oil,mayai,Nyama,parachichi,korosho nk Naomba unipe ushuhuda umepungua kilo ngapi kwa kujinyima kula mafuta.
Leo hii watu wengi wanatoa ushuhuda jinsi gani wamepungua uzito kwa juhudi ndogo tu, ya kufuata mpangilio wa mlo wetu unao lenga kupunguza vyakula vya wanga,kuongeza vyakula vya mafuta na ulaji wa mboga za majani kwa wingi na protini kwa wastani.
Nafurahi sana mnatoa matokeo makubwa.
Watu wengi watakwambia unakula sana, watu wengi watakwambia uzito ni wakurithi lakini hayo yote sio kweli adui yako ni vyakula vya sukari na wanga na sio hata vyakula vya mafuta.
Leo hii nikitamka "Kula vyakula vya mafuta bila woga ,kila mtu anajing'ata ulimi kwa mshangao" Inasitisha mshangao huo ungenionesha umepunguza kilo kiasi gani! Umekuwa ukivikwepa kwa njia zote lkn bado kila mwezi kilo zinapanda.
Jiulize tatizo ni MAFUTA AU KITU GANI?
Utasikia au utaona vyakula vimeandikiwa "Low Fats" au "No Fats" hio ni ishara kuwa sio vyakula kama unataka mwili wako uanze kuunguza mafuta badala ya kuhifadhi pekee.
Unapotaka kupunguza uzito ufanye mwili wako uwe wenye kuvunja vunja viini lishe na sio kuhifadhi tena.
"Catabolic process should be higher than Anabolic process"
Inaonekana kama nakupotosha lakini wachache ambao wamefutilia lishe hii wamefikia pazuri kabisa na shuhuda kibao.
Ulaji wa Vyakula vya wanga kwa wingi vinasababisha mambo makuu haya
-Sukari kupanda kwa kasi
-Insulin nayo kuongezeka kama mwitikio kuja kuhifadhi sukari iliyozidi kiwango cha matumizi stahiki ktk mfumo wa mafuta [TGA]
-Ulaji hovyo [Njaa za mara kwa mara] kwa sababu kiwango cha insulin kipo juu.
-Kuongezeka kwa mafuta [nyama uzembe] sehemu za kuhifadhia mafuta yanayohifadhiwa na homoni ya insulin.
Baada ya kusema hayo, inaonesha kuwa ulaji wa vyakula vya wanga kupita kiasi utaendelea kunenepa hata kama unajinyima kula vyakula vya mafuta.
ZINGATIA;
Hivi unajua kwamba dhana ya kupunguza vyakula vya mafuta na kuongeza vyakula vya wanga ni mtitiriko wa kisayansi ili kuufanya mwili wako ufanye kazi katika kiwango stahiki bila kukosa nishati ya mwili yakutosha.
Basi katika lishe hii nimekuwa nikishauri kuwa kama unataka kuifuata
"Hakikisha unapopunguza wanga Ongeza vyakula vya mafuta" Hio ndio principle ya Lishe katika sayansi ya kupunguza uzito.
Lengo ni kuhakikisha kwamba umepunguza wanga kwa kiasi kikubwa na utapata matokeo haya.
-Hakuna sukari ya ziada itakayo hifadhiwa ktk mfumo wa mafuta
-Baada ya mmwili kumaliza kutumia mafuta uliyokula basi mwili utaanza kuzalisha nishati ya mwili kwa kutumia mafuta yaliyohifadhiwa [yanayotengeneza nyama uzembe]
Hapo ndipo mwili wako utauzoesha kutumia Ketone kutoka kwenye uungazaji wa mafuta na utajipatia nguvu imara zaidi hata ya vyakula vya wanga.
FURAHIA MPANGILIO WA MLO WANGU KILA SIKU UAMKAPO KWA KUUNGANA NAMI FACEBOOK KUHAKIKISHA KILA MTU ANAISHI BILA KITAMBI KWA KUOUNGUZA KITAMBI NA KILO KIAFYA BILA GHARAMA TOFAUTI NA MLO WAKE WA KILA SIKU AMBAO UTATAKIWA KUPANGILIA
Facebook: Dr Boaz Mkumbo MD.
Asanteni

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top