Nadharia ya Charles Darwin inaweza kueleza kwa urahisi sababu ya tausi dume kukoga mkia wake. Tausi dume akiwa na mkia mrefu wenye rangi nyingi, atavutia zaidi tausi jike. Lakini Bw. Darwin hakuweza kueleza sababu ya kulia kwa binadamu, ila aliwahi kusema, binadamu alipata uwezo wa kulia kwa bahati sana. Bila shaka Bw. Darwin alikosea.
Nadharia inayokubaliwa na watu wengi zaidi siku hizi ni kwamba machozi ni ishara ya mawasiliano, yanatokana na uwezo wa kuomba msaada wa mamalia.
Lakini jambo lisiloweza kuelezwa kwa urahisi ni kwamba, tunapolia tutaonesha hisia zetu kwa maadui, hiki ni kitendo hatari, kwa nini bado tunalia?
Mwanasaikolojia wa Uholanzi Ad Vingerhoets alieleza sababu ya kulia. Ingawa katika hali kadhaa kulia kutaleta hatari, lakini kitendo hiki bado ni salama zaidi kuliko kupia kelele kubwa kwa njia nyingine, hasa watu wanapowasiliana kwa karibu. Kwa mfano mtoto mchanga akitoa machozi, mama atajua hana furaha.
Maneno ya Bw. Vingerhoets ni sahihi, lakini kulia hakuhusiani na mahitaji ya msaada tu. Mtaalamu wa utamaduni na historia Bw. Thomas Dixon alisema, machozi yanatokana na akili ya binadamu. Binadamu wanatoa machozi yenye maana tofauti kuendana na hali tofauti.CHANZO CRI SWAHILI
Post a Comment