Shirika la polisi wa Interpol limetangaza kuwa limetia mbaroni washukiwa 376 wa baishara haramu ya bidhaa zinazotengenezwa kutokana na wanyamapori katika mataifa mbali mbali barani Afrika.
Katika taarifa yake siku ya Jumatano, Interpol ilisema kuwa operesheni hiyo ambayo iling'oa nanga Januari mwaka huu iliweza kunasa tani 4.5 ya bidhaa hizo haramu. Operesheni hiyo iliyodumu kwa muda wa miezi 10 ilifanywa nchini Ethiopia, Kenya, Malawi, Mozambique, Namibia, South Africa, Sudan, Swaziland, Tanzania, Uganda na Zambia.
Post a Comment