Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Korea Kusini inashuhudia viwango vya juu zaidi vya kujiua duniani.
Idadi kubwa ya wafanyikazi nchini humo hukumbwa na msongo wa mawazo.
Ni kwa sababu hiyo ndiyo makampuni mengi yameanza kuweka mikakati ya kukabiliana na matatizo yanayochangia takwimu hiyo.
Kampuni moja imewaagiza wafanyikazi wake wakabiliane na kifo.
Kivipi labda unajiuliza?
Makampuni hayo,yanawashawishi waajiriwa wao waigize wanashiriki mazishi yao wenyewe !


Katika jumba moja la kisasa wafanyikazi wa kampuni moja inayoendesha shughuli ya usaili na uajiri wa wafanyikazi wanaomboleza vifo vyao.
Wakiwa wamevalia mavazi meupe, wanaandika barua yao ya mwisho kwa wapendwa wao.
Huku wakibubujikwa na machozi wafanyikazi hao wanatumbukia katika majonzi tele,,wengine hata wanaonekana wakiangua kilio kwa uchungu wa kumpoteza mpendwa wao,,,
Taswira sawasawa na ile inayoshuhudiwa mazishini.
Wanaketi mbele ya picha zao zilizofungwa na tepe nyeusi ,,,,mara kilio tena kinasikika kilio cha kwi kwi kwi ,,,,machozi tena yanatiririka .
Wengine wanakumbatia picha zao kana kwamba wanaaga ama kutoa mkono wa buriani.
Mkono wa kushoto ,kuna jeneza lililoko wazi.
Kilele cha maombolezi hayo ni wao wenye kusimama wima na kunyamaa kwa muda.
Kisha wanaingia ndani ya majeneza hayo ya mbao na kulala chali.
Kisha mtu mmoja aliyevalia magwanda meusi anawakaribia.
Huyo ndiye malaika wa kifo.
Ndiye anayechukua uhai wao.
Mkonononi ana nyundo na msumari.
Anakaa mfano wa kivuli tu.
Anafunga jeneza na mara anagonga misumari.
Wakiwa humo ndani wanafikiria kuhusu maisha yao, wanapiga msasa matukio maishani mwao.

Kimsingi wanakufa.
Kampuni hiyo inalenga kuchochea mtagusano baina ya wafanyikazi wake na pia ni funzo kwao kudhamini upya maisha yao.
Kabla ya 'kufa' wanaoneshwa video za watu ambao wanakaribia na kifo kutokana na magonjwa.
Kwa mfano mhasiriwa wa saratani ambaye anaishi siku zake za mwisho, au mtu aliyezaliwa bila mikono na miguu lakini amejifunza kuogelea .
Haya yote ni kwa dhamira ya kuwashawishi wakubali maisha yao yalivyo na kuwa kila mtu anachangamoto moja au zaidi maishani.
Muasisi wa mpango huu mpya Jeong Yong-mun anawataka wakubali maisha na changamoto zake.
Jeong ndiye muasisi wa kituo hicho cha Hyowon Healing Centre.
Washirika katika shughuli hiyo leo,walitumwa na mwajiri wao.

Lakini bwana Jeong Yong-mun anasema kuwa mtaala wake ni wa kipekee na unalenga kukwamua mfumo wa mawazo na maktaba ya watu.
Nia yake kimsingi ni kuwasaidia watu kufikiria zaidi ya upeo wa mawazo yao.
Kwa sasa matokeo yake hayajabainika ila kwa wale ambao wamepitia mpango huo wanausifia sana.
"baada ya kufunikiwa ndani ya jeneza ,niligundua kuwa ninastahili kuanza maisha yangu upya''
''Niligundua kuwa ninastahili kufungua ukurasa mpya maishani mwangu ''alisema bwana Cho Yong-tae 'alipofufuka' kutoka ndani ya jeneza.
"Niligundua kuwa kwa hakika nimekuwa nikiishi maisha yangu kwa njia isiyoridhisha hata kidogo''
''Nimefanya makosa mengi mno'', anaongezea.

Muajiri wake Park Chun-woong anaamini ni wajibu wa kila muajiri kujali maisha ya wafanyikazi wake ilikuimarisha viwango vya uzalishaji wao.
Yeye husisitiza kuwa wafanyikazi wake wajinyooshe kila siku asubuhi wanapoingia kazini, kisha wanaangua kicheko.
Watafiti wa maradhi yanayoathiri akili wanasema kuwa njia zote zinahitajika kujaribiwa ilikupunguza idadi ya watu wanaojitia kitanzi nchini Korea.
Taifa hilo linashinikiza kizazi chao kiboreshe matokeo ya mitihani na kuongeza mafanikio yao.
Ilikuthibitisha wamepiga hatua kuliko kizazi kilichotangulia.
Kwa mfano wazazi wengi hufunga na kuomba ili wanafunzi wao wafaulu katika mitihani.
Si aghalabu kuwa basi kuwa wakorea wengi wanakabiliwa na msongo wa mawazo.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top