Michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) mzunguko wa pili unaendelea leo kwa mchezo mmoja kuchezwa mmoja katika uwanja wa Majimaji mjini Songea kati ya JKT Mlale dhidi ya Mighty Elephant.
Kesho Jumatano kutakua na michezo miwili, Kariakoo ya Lindi watawakaribisha Mshikamano FC katika uwanja wa Ilulu – Lindi, Disemba 24 Njombe Mji watakua wenyeji wa Green Warriors katika uwanja wa Sabasaba mjini Njombe, na Pamba FC watacheza dhidi ya Alliance uwanja wa CCM Kirumba.
Ijumaa siku ya sikukuu ya Krisamsi Lipuli FC watawakaribisha Kurugenzi katika uwanja wa Wambi Mafinga.
Mzunguko huo wa pili unatarajiwa kumalizika Disemba 29 mwaka huu kwa michezo minne, Wenda FC v Kimondo (Sokoine), Mji Mkuu (CDA) v Singida United (Jamhuri), Mvuvuma v JKT Kanembwa (Tanganyika), Abajalo FC v Villa Squad (Karume)
Timu saba za Ashanti United, Burkinafaso, Geita Gold, Friends Rangers, Madini FCM, Panone na Rhino Rangers zimeshakata tiketi ya kucheza mzunguko wa tatu wa Kombe la FA mwezi Januari 2016, pamoja na timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom.
Bingwa wa michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) ataiwakilisha Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF CC) mwaka 2017.
Post a Comment