Mkuu wa Wilaya ya Chunya Elias John Tarimo akizindua Mradi wa Kisima cha Maji Kijiji cha Ngwala Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya.
Baadhi ya Wananchi wakishuhudia uzinduzi wa Mradi wa Maji Kijiji cha Ngwala Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya.
Na
Ezekiel Kamanga ,Mbeya,Jamiimojablog
Serikali
WIlayani Chunya Mkoani Mbeya kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wameendelea
na jitihada mbalimbali katika kuhakikisha wanatatua changamoto ya ukosefu wa
maji wilayani humo.
Hatua
hiyo inakuja kufuataia kampuni ya Peak
Resource limited ambayo hujihusisha na utafiti wa madini adimu chini ya ardhi
yanayopatikana katika kata ya ngwala wilayanii chunya mkoani mbeya
kuchimba visima viwili vya maji vyenye thamani ya shilingi milioni 16.
Akizungumza
wakati wa makabidhiano ya visima hivyo Mkuu wa Wilaya ya Chunya Ndugu Elias
Tarimo amesema hatua ya kampuni huyo
inayojihusisha na utafiti
wa madini kuamua kuchimba visima hivyo kwa lengo la kuwasaidia wananchi ni
jambo jema nalinalotakiwa kuungwa mkono na wananchi hao.
Amesema
katika kuunga mkono jitihada hizo wananchi hao hawana
budi kutunza miundo mbinu hiyo waliojengewa kwani wakiiharibu watarudi katika
adha ya shida ya maji walikuwanayo hapo awali na kwamba waendeleze ushirikiano
bora na kampuni hiyo.
Akisoma tarifa fupi ya ujenzi wa miradi
mbalimbali waliojenga katika kata hiyo meneja mradi wa Peak Resource
limited Patrick Ochieng amesema miradi waliojenga ni visima viwili
vilivyogharimu milioni 16kila kimoja unjezi wa nyumba ya mwalimu
iliyogharimu shilingi milioni 55 na ujenzi wa eneo la kupumzikia wagonjwa
katika kituo cha Afya cha Ngwala iliyogharimu shilingi milioni 7
vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 94.
Ochieng
alindelea kueleza kuwa kwa sasa Kampuni yao ipo katika hatua za mwisho za
utafiti na kwamba wanafwatilia leseni ya uchimbaji madini na kibali kutoka
nemki ili kuanza uzalishaji na kwamba mgodi huo unauwezo wa kudumu kuchimbwa
kwa miaka 40.
Aidha
baadhi ya waliohudhuria katika sherehe za uzinduzi wa miradi ni pamoja na
Mwenyekiti wa kijiji cha Neston Simoni na Diwani wa Kata ya Ngwala Donard
Maganga ambao walisema wamefurahishwa na kile kinachofanywa na kampuni hiyo
kwani wanajenga miradi bora kwa kutumia gharama nafuu.
Maganga
aliwataka wakazi wa Ngwala kuiga mfano wa kampuni hiyo kwani nalisema nyumba
waliojenga ya shilingi milioni 55 ukiweka Mkandarasi wangeweza kujenga kwa
shilingi milioni 100 hivyo alisema mfano wa kampuni hiyo unapaswa kuigwa ili
kuondoa ufisadi katika jamii yetu.
Kwaupande
wa wananchi waliokuwepo hapo walishukuru kampuni hiyo kwa kupunguza adha
walizokuwa nazo katika Kata yao kwani kwasasa wamekuwa na matumaini wa kupata
walimu ambao watafundisha watoto wao katika mazingira yalio bora kutokana na
uwepo wa nyumba bora ya Mwalimu ukilinganisha na hapo awali walikuwa wanakosa
eneo la kujihifadhi,alisema Raisoni George.
Vile
vile Elizabeti Yusuph mkazi wa ngwala alisema wao kama wakinamama walikuwa
wachelewa kufanya shughuli za shambani kutokana na kufwata maji umbali mrefu
kwani kutokana na uwepo wa mrado huo wa maji utarahisisha shughuli nyingine.
Mwisho.
Post a Comment