Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
muhongo+px
Serikali imesimamisha shughuli za uchimbaji wa Makaa ya Mawe ya Kampuni ya Off- Route Technology iliyopo Kyela ikiwemo kukamata vifaa vya uchimbaji na kuwekwa chini ya uangalizi wa Mkoa wa Mbeya hadi hapo uchunguzi dhidi ya uhalali wa kampuni hiyo kuchimba makaa utakapokamilika.
Hatua hiyo inafuatia ziara ya Waziri wa Nishati na Madini, Prof Sospeter Muhongo kutembelea mgodini hapo na kubaini kuwa, kampuni hiyo inachimba makaa bila kuwa na leseni halali ya uchimbaji madini.
Aidha, Prof. Muhongo ameitaka kampuni hiyo kulipa kodi zote za Serikali ikiwemo inazodaiwa na Halmashuri tangu ianze kufanya shughuli za kuchimba. Aidha, ili kujua undani wa suala hilo, Prof. Muhongo ameitisha kikao kifanyike kati ya mgodi huo , Wizara ya Nishati na Madini, Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania ( TMAA), Ofisi ya Madini Kanda ya Kusini Magharibi, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kyela, tarehe 18 Januari, 2016 

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top