Waziri wa Ufaransa alisema kuwa mashambulizi dhidi ya kundi la Islamic State yalianza siku ya Jumatatu na kufikia siku ya Alhamisi ngome saba za waasi hao katika mji wa Mosul zilikuwa zimeharibiwa.
Mawaziri wa ulinzi kutoka nchi saba za uanachama wa muungano unaoongozwa na Marekani (Ufaransa, Marekani, Australia, Ujerumani, Uingereza, Italia na Uholanzi) watakutana siku ya Jumatano mjini Paris, Ufaransa, kujadili jinsi ya kuongeza jitihada zao za kukabiliana na Islamic State nchini Iraq na Syria, Le Drian alisema.
(picha:AP)China Xinhua News
Post a Comment