Meneja wa Huduma Mbadala wa Benki ya CRDB, Joseph Wite (katikati), akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya Jitegemee JKT, Brigedia Jenerali mstaafu Lawrence Magere (kushoto), hundi yenye thamani ya sh.milioni 2.5 kwa ajili ya kusaidia kujenga mifumo ya maji shuleni hapo katika Mahafali ya 22 ya kidato cha sita yaliyofanyika Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkuu wa Shule hiyo, Luteni Kanali Robert Kessy.
Wazazi na walezi wa wanafunzi hao wakiwa kwenye mahafali hayo.
Viongozi mbalimbali wakiwa na mgeni rasmi wakielekea ukumbini.
Maandamano ya wanafunzi hao yakielekea ukumbini.
Wimbo wa Taifa ukiimbwa.
Bendi ya JKT ikitumbuiza.
Wimbo maalumu wa shule ukiimbwa.
Wanafunzi wa kidato cha sita wakiwa kwenye mahafali hayo.
Burudani zikiwa zimepamba moto.
Mkuu wa Shule, Luteni Kanali, Robert Kessy akizungumza kwenye mahafali hayo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya Jitegemee JKT, Brigedia Jenerali mstaafu Lawrence Magere akizungumza kwenye mahafali hayo.Meneja wa Huduma Mbadala wa Benki ya CRDB, Joseph Wite (katikati), akizungumza katika mahafali hayo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule, Brigedia Jenerali mstaafu Lawrence Magere (kushoto), akimkabidhi hundi iliyotolewa na CRDB, Mkuu wa shule hiyo, Luteni Kanali Robert Kessy.
Mkuu wa Shule akimkabishi cheki hiyo, Meja Rehema Wanjara Msarifu wa Shule. Wengine kutoka kulia ni Makamu Mkuu wa Shule hiyo na Utawala, Kapteni Benitho na Mjumbe wa Bodi ya Shule, Sebastian Inosh.
Kwaito likiwa limepamba moto.
Hapa mwanafunzi Khalifa Chege aliyekuwa namba moja katika masomo akikabidhiwa zawadi.
Mwanafunzi Ibrahim Pazi aliyeshika nafasi ya pili katika masomo akikabidhiwa zawadi.
Dotto Mwaibale
BENKI ya CRDB imetangaza ajira kwa wanafunzi wa kidato cha sita katika Shule ya Sekondari ya Jitegemee JKT watakao pata divisheni one ya pointi tatu baada ya kufanya mtihani wa taifa.
Ofa hiyo ilitolewa na Meneja wa huduma mbadala wa Benki ya CRDB Joseph Wite kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo Dk. Charles Kimei katika mahafali ya 22 yaliyofanyika shuleni hapo Dar es Salaam jana.
Katika hatua nyingine Wite amewataka wanafunzi hao kutumia fursa ya ajira katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kwani uwezekano upo endapo watafanya bidii katika masomo yao.
Alisema ni wakati wa vijana kuchangamkia fursa za ajira katika jumuiya ya Afrika Mashariki ili kuweza kufikia malengo na kuondokana na dhana ya kwamba hakuna ajira nchini.
"Pamoja na kwamba vijana wengi wanahofia kuajiriwa nje ya nchini kutokana na mambo mbalimbali ikiwemo kuogopa kwamba hawawezi kukidhi vigezo lakini mimi napenda kuwatoa hofu hiyo kwamba hata kama kiingereza huwezi kiswahili utashindwa kufundisha,"alisema Wite.
Aliwataka wanafunzi hao kuhakikisha kwamba wanajiepusha na matendo mabaya ambayo yatapelekea kujiunga na madawa ya kulevya na kuhatarisha maisha yao.
Alisema mtu anapojiunga na madawa ya kulevya ana uwezekano mkubwa wa kupata magonjwa ya kuambukiza ikiwemo ukimwi.
"Janga la ukimwi halichagui mwenye nacho au asiye nacho ukicheza unahatarisha maisha hivyo ni vyena mjihadhari nalo ili muweze kufikia malengo,"alisema.
Hata hivyo aliendelea kusema kuwa benki hiyo inachangia kwa kutambua asilimia moja ya faida wanayoipata kwa mwaka kwa sekta zinazopewa ikiwemo elimu na afya.
Pia alisema benki hiyo itaisaidia shule hiyo milioni 2.5 kwa ajili ya kuboresha mfumo wa maji safi.
Mkuu wa Shule hiyo Luteni Kanali Robert Kessy alisema wanafunzi wanaohitimu katika mahafali hayo ya 22 ni 558.
Alisema wamewalea wanafunzi hao katika maadili mazuri pamoja na kuwafundisha nyezo zote hivyo wanatarajia kwamba watafanya vizuri na kuwa mabalozi wazuri katika jamii.
Mmoja ya wazazi waliohudhuria mahafali hayo Hamisa Athumani aliipongeza shule hiyo kwa kufundisha masomo ya ukakamavu kwani yamewajengea uwezo wa kujiamini na kuwa na nidhamu.
Post a Comment