Katibu Mkuu wa Chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi (katikati), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo wakati akiwapokea waliokuwa viongozi wa Chama cha UDP, waliokihama chama ambao ni Salum Makunganya aliyekuwa Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Mtwara na Mkurugenzi wa Uchaguzi Taifa na Mjumbe wa Halmshauri Kuu na Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Dar es Salaam na aliyekuwa Mjumbe wa Halmshauri Kuu ya chama hicho , Joachim Mwakitiga waliotangaza kujiondoa katika chama hicho na kujiunga CCK jijini Dar es Salaam leo asubuhi mbele ya waandishi wa habari.
Mwenyekiti wa Wanawake CCK Taifa, Salama Juma (kulia), akizungumza wakati wa kuwapokea viongozi hao. Kushoto Salum Makunganya aliyekuwa Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Mtwara aliye hamia CCK.
Katibu Mkuu wa Chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi (kulia), akimkabidhi kadi ya chama hicho aliyekuwa Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Dar es Salaam, Joachim Mwakitiga aliyejiunga na chama hicho na aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Mtwara, Salum Makunganya Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi (kulia), akimkabidhi kadi ya chama hicho aliyekuwa Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Mtwara, Salum Makunganya aliyehamia chama hicho.
Na Dotto Mwaibale
CHAMA cha United Democratic Party (UDP) kinachoongozwa na Mwenyekiti wake wa Taifa, John Momose Cheyo, kimepata pigo baada ya wenyeviti wawili wa mikoa ya Mtwara na Dar es
Salaam kukihama na kujiunga na Chama Cha Kijamii (CCK).
Viongozi waliokihama chama hicho ni Salum Makunganya ambaye alikuwa Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Mtwara, Mkurugenzi wa Uchaguzi Taifa na Mjumbe wa Halmshauri Kuu ya chama hicho na Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Dar es Salaam na Mjumbe wa Halmshauri Kuu, Joachim Mwakitiga waliotangaza kujiondoa katika chama hicho na kujiunga CCK leo jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa
habari.
Wenyeviti hao baada ya kujitoa walikabidhi kadi zao za UDP kwa Katibu Mkuu wa CCK, Renatus Muabhi ambaye naye aliwakabidi kadi ya CCK na kuwatangaza rasmi kuwa wanachama wa chama hicho.
Makunganya alikabidi kadi yake ya UDP yenye namba 4544 na kukabidhiwa ya CCK namba 1597 huku Mwakitiga akibidhi kadi yake ya UDP namba 2852 na kukabidhi ya CCK yenye namba 01599 katika tukio lililofanyika ofisi za CCK.
Wakizungumzia sababu zilizowafanya wajitoe UDP walisema ni kutokana na chama hicho kutokuwa na mwelekeo wa kimaendeleo ambacho kwa zaidi ya miaka sita viongozi wake wa kitaifa hawajaitisha mikutano ukiwamo wa Halmashauri Kuu ya Taifa na Kamati Kuu.
Walisema sababu nyingine ni kwamba viongozi wa kitaifa wa UDP wamekigeuza chama hicho kama kampuni binafsi ambapo wamekuwa wakitoa maamuzi mbalimbali ambayo hayajaamuliwa na wanachama kwenye vikao .
“Nyie waandishi si mnaishi Dar es Salaam tangu lini mlishaona Mwenyekiti wa Taifa wa UDP, John Cheyo akiitisha hata mkutano wa hadhara hapa Dar es Salaam kuzungumzia mambo mbalimbali ya chama na taifa kwa ujumla kama vinavyofanya vyama vingine…jibu ni hakuna, UDP inabuka tu wakati wa uchaguzi na tena kwenye eneo moja tu,”alisema Mwakitiga.
Muabhi akizungumza baadhi baada ya kuwakabidhi kadi wenyeviti hao alisema CCK inawapokea kwa mikono miwili viongozi hao na kwamba wakiwa ndani ya chama hicho wataona utofauti na vyama vingine kwa kuwa chama kimejiwekea misingi ya kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi.
Muabhi aliitaka serikali kulitazama upya suala la vikao vya Bunge kutotangazwa kwenye vyombo vya habari kwa kuwa kufanya hivyo kunawanyima haki wananchi ya kupata habari na hivyo kushindwa kujua nini kinaendelea Bungeni.
“Serikali ijitathimini, wananchi wasipojua nini kinaendelea Bungeni kuna haja gani kwa wabunge ambao ndio wawakilishi wa wananchi kwenda Bungeni, wananchi watajuaje kama wawakilishi wao wamezifikisha kero zao serikalini,”alisema.
Mwenyekiti wa Wanawake CCK Taifa, Salama Juma, alisema ujio wa wanachama hao wapya ambao ni wakongwe katika siasa na hivyo CCK itajifunza mambo mengi kutoka kwao.
Post a Comment