Mwenyekiti
wa Kampeni ya Okoa Tembo Bw. Shubert Mwarabu (katikati) akielezea kuhus
Kampeni yao ya kuokoa Tembo wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari
uliofanyika leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Jijini Dar es
Salaam. Kushoto ni Mjumbe wa Kampeni hiyo Bw. Lameck Mkuburo pamoja na
Bw. Arafat Mtui (wa kwanza kulia).
(PICHA NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO)
……………………………………………………………………………………………………………………………
Na Anitha Jonas – MAELEZO- Dar es Salaam.
Taasisi isiyo ya kiserikali ya
Okoa Tembo Tanzania imemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt.John Pombe Magufuli kuteketeza ghala la meno ya tembo liliopo nchini
kufuatia Tanzania kusaini mpango wa kuwalinda Tembo mwaka 2014 unaozuia
uuzaji wa meno ya Tembo kwa muda wa miaka 10.
Ombi hilo limetolewa leo jijini
Dar s Salaam na Mwenyekiti wa Kampeni ya Okoa Tembo Tanzania Bw.Shubert
Mwarabu alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Barua ya
Wazi waliyomwandikia Mheshimiwa Rais.
Amesema Tanzania inafungwa na
mkataba wa kimataifa wa biashara juu ya viumbe vilivyo hatarini kutoweka
(Convetion on International Trade in Endangered Species-CITES) ambao
unabainisha kuwa Tanzania kwa sasa haiwezi kuuza ghala lake la meno ya
Tembo.
Amesema uhifadhi wa meno hayo
unaigharimu serikali fedha nyingi na kufafanua kuwa kwa sasa Tanzania
ina hifadhi kubwa ya meno ya Tembo yaliyokamamwa kutokana na ujangili.
“Tunampongeza Mheshimiwa Rais kwa
kasi yake ya utendaji tangu kuchaguliwa kwake,tunamuomba atekeleze
lengo la tatu la kampeni yetu ya Okoa Tembo wa Tanzania kwa kuliteketeza
hadharani ghala la meno ya tembo,tunaona hakuna haja ya kuendelea kuwa
na ghala hili” amesema Bw.Mwarabu.
Amesisitiza kuwa ombi lao kwa
Rais kutaka ghala la meno ya Tembo liteketezwe kutasidia kutuma ujumbe
mzito kwa majangili na wafanyabiashara kuwa meno ya Tembo hayana thamani
ya pesa kiasi cha serikali kuona wepesi kuteketeza hazina hiyo.
“ Tunataka ieleweke kwamba
kuharibu ghala la meno ya Tembo kunatuma ujumbe mzito kwa majangili na
wafanyabiashara kuwa meno ya Tembo hayana thamani ya pesa na kuwa
ujangili ni kosa la jinai lisilokubalika” Amesisitiza.
Amesema ipo haya ya Tanzania
kuunga mkono mpango wao wa kuteketeza ghala la meno ya Tembo kama
inavyotarajiwa katika nchi ya Kenya ambayo inatarajia kuteketeza ghala
lake la meno ya Tembo hadharani Aprili 30 mwaka huu.
Amezitaja nchi ambazo zina mpango wa kuchukua hatua kama ya Kenya kuwa ni Ethiopia,Chad,Gabon, Mozambique na Congo.
Naye mmoja wa wajumbe wa Kampeni
ya Okoa Tembo wa Tanzania Bw.Arafat Mtui akizungumza katika mkutano huo
amesisitiza kuwa kuendelea kuwepo kwa ghala hilo nchini Tanzania
kunawapa moyo wafanyabiashara haramu wa meno hayo kuona kuwa ipo siku
biashara hiyo itaendelea tena.
Amesema Kampeni yao ya Okoa Tembo
wa Tanzania inaendelea kusisitiza kuwa kuwa hatma ya Tembo wa
Tanzania iko mikononi mwa watanzania, hivyo ni vema Serikali
ikashirikiana na wadau mbalimbali kuchukua hatua madhubuti kuokoa
viumbe hao walio hatarini kutoweka kwa ajili ya kizazi cha sasa na
vizazi vijavyo.
Post a Comment