Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Butusyo Mwambelo akionyesha silahaaina ya panga ambalo linadaiwa kutumiwa na majambazi hao . |
Silaha mbalimbali zilizo kamatwa katika tukio la kuuwawa kwa majambazi wilayani Chnua mkoani mbeya April27 mwaka huu. |
Na EmanuelMadafa,(Jamiimojablogu-Mbeya)
JESHI la Polisi mkoani Mbeya
limewauwa watu watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wakati wa
kurushiana rasasi.
Kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Butusyo Mwambelo amesema
tukio hilo limetokea April 27 mwaka huu saa 2 usiku , huko katika kijiji cha Matundasi
Wilayani Chunya Mkoani Mbeya .
Amesema watu watano wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wakiwa na bunduki
moja ya aina ya SMG yenye namba 1996 AFU 1120 na risasi 26 kwenye magazine ,
walifika kijijini hapo kwa lengo la
kufanya uhalifu kwenye duka la jumla la kuuzia vinywaji mali ya Ndugu Hamis Mkazi wa eneo hilo la
Matundasi Chunya..
Kamanda Mwambelo , amesema watu hao ambao miili yao imehifadhi
kwenye chumba cha mochwari katika hospitali ya wilaya ya Chunya , majina na
makazi yao bado hayajajulikana.
Akifafanua, amesema taarifa za siri kutoka kwa raia wema zilifikia
jeshi la polisi na ndipo askari polisi walipofika kwenye eneo la tukio.
“Baada ya polisi kufika katika eneo la tukio watu hao walistuka kuwa wanafuatilwa na askari
polisi na hivyo kuanza kukimbia kuelekea kijiji cha Matondo kwa kutumia pikipiki yenye namba za usajili MC
761. AFS aina ya Sanlag yenye rangi nyeusi”,amesema Mwambelo
.
Amesema walipoona Polisi wanawakaribia walianza kurusha risasi hovyo hewani ambapo jambazi mmoja
alijeruhiwa baada ya kupigwa risasi mguuni na tumboni na kufariki dunia ambapo
majambazi wanne walifanikiwa kutoroka .
Amesema kutokana na hali hiyo jeshi hilo la polisi lilianzisha
msako usiku huo na kufanikiwa kuwaua majambazi wengine wawili ambao huku wengine wakitoroka ambapo msako
mkali unaendelea ili kuwakamata wahalifu hao.
Amesema katika eneo la tukio, ilipatikana
bunduki moja aina ya SMG yenye namba 1996 AFU
1120 ikiwa na risasi 27 kwenye
magazine. Pia pikipiki iliyokuwa iantumiwa na majambazi hayo, iliwezea
kupatikana pamoja na panga .
Mwambelo alitoa wito kwamba
wananchi waendelee na moyo huo huo wa kuwafichua watu wanaowatilia shaka ili
waweze kudhibitiwa mapema kabla ya kufanya uhalifu sanjali na kufika katika
hospital ya wilaya ya Chunya kwa lengo la kufanya utambuzi wa miili ya majambazi
hao kwani majina yao bado hayajatambulika.
Mwisho
Post a Comment