MKuu Mkoa wa Mbeya Amos Makalla azungumza na Wamachinga Mwanjelwa MKUU WA MKOA ATINGA SOKO LA MWANJELWA NA KUAGIZA WAFANYABIASHARA PEMBEZONI MWA SOKO NA WAMACHINGA KUINGIA NDANI YA SOKO |
- Atoa siku Tano kwa watendaji wa soko kuwapa maeneo
- Asema utaratibu wa kuwajengea vibanda utachukua muda
- Ahaidi kukaa na CRDB kupunguza bei YA vyumba
- wananchi wafurahia uamuzi huo utasaidia SOKO kukaa wateja
MKUU wa Mkoa wa Mbeya amefanya ziara ya kustukiza SOKO la Mwanjelwa kujionea haki YA biashara sokoni hapo na kugundua SOKO hilo kupooza kwa kukosa wateja na sababu ikiwa ni bei kubwa YA vyumba na pia wateja kukos slabs kwa wateja
Ili kukabiliana na tatizo hilo amemwagiza mkurugenzi wa jiji kuwaingiza ndani ya eneo la wazi la SOKO wamachinga wote na wanaofanya biashara pembezoni mwa soko kwani kufanya hivyo kutaongeza wateja na soko kuchangamka na pia italeta ushindani ulio Sawa kwani walio nje YA soko hawalipi ushuru na wanasababisha msongamano. " Mkurugenzi nimesikia madiwani wanawakwamisha kuwasaidia wananchi Hawa nilipowaondoa kule Kabwe maeneo hatarishi walipinga, nilipofuatilia ufisadi wa soko hili walipinga wamesahau kabisa kuwa Hawa ndiyo waliowachagua kwa kuwa mimi ndiyo kiongozi wa serikali tekeleza agizo hili ktk siku 5 ili tuwasaidie watu Hawa "
Kuhusu kodi YA vyumba amehaidi kukaa na benki YA Crdb tarehe 15 septemba ili kupunguza kodi na riba ili kuleta u nafuu kwa wapangaji
Post a Comment