Add capt |
Mwandishi wa Makala hii Ndugu Innocent Ng'oko |
Mji wa ujiji iliopo katika mkoa wa Kigoma upande wa Magharibi mwa Tanzani ni eneo mbalo lina umhimu mkubwa kutokana na historia lukiki ikiwepo ya wapelelezi akina Henry Morton Stanley na Dr. David livingstone waliokutana chini ya muembe Novemba, 10,1871 na sehemu ya eneo hilo kwa sasa yamejengwa makumbusho yenye vivutio vya kipekee zikiwemo tamaduni za kabila la waha wa mkoa wa Kigoma.
Mji wa Ujiji ni moja ya miji ya kale sana nchini Tanzania ambayo ilikuwa ni moja ya vituo vya kibiashara kwa wakoloni(biashara ya watumwa na shanga) na ni eneo ambalo wapelelezi akina Richard Burton na John Speke walikuwa wa kwanza kufika katika pwani ya Ziwa Tanganyika na kuanika ubaya wa biashara ya utumwa na pembe za ndovu na kufanikiwa kukomeshwa kwa biashara ya utumwa mwaka 1873 .
Unapofika katika mji wa Ujiji utastajambishwa kuona miti ya miembe ya kale iliyopandwa kwa ustadi mkubwa na kufanya kuwa na mvuto usiochosha kwa mgenini yeyote na eneo hilo la miti ya miembe lina kinvuli kizuri sana nyakati za mchana.
Pia unapokuwa katika eneo la Ujiji ustashuhudia majengo ya kale sana ( enzi za kikoloni) na baadhi ya majengo hayo ya zamani ni shule ya msingi Karuta ambapo zamani ilikuwa ikifahamika kama seminari ya Ujiji ambayo ilijengwa na wakoloni wa Kijerumani.
Unapoingia ndani ya makumbusho hayo ya Dr. David livingstone utapata simulizi za kusisimua za kabila la waha wa mkoa wa kigoma na tamaduni zao zikiwemo ngoma za jadi,zana za shughuri za uvuvi katika ziwa Tanganyika na maisha yao mengine ya kila siku pamoja na historia za wapelelezi akina Henry Morton Stanley , Dr. David livingstone na Tip tip.
Wenyeji wa mji wa Ujiji wanasifika sana kwa usafi,si jambo rahisi sana kumkuta mwenyeji wa mji huo akiwa mchafu na katika makumbusho hayo utakuta kumbukumbu za viatu vya miti vilivyokuwa vikitumiwa na waha.
Pembezoni mwa jengo la makubusho hayo kuna ufukwe mzuri sana wa Forodhani ambapo kwa mgeni yeyote utaweza kufurahia madhari nzuri sana ya ziwa Tanganyika na shughuri za uvuvi zinazoendelea katika ziwa hilo.
Na unapofika kigoma bila kula samaki aina ya migebuka bado hujafika kigoma,pia utakutana na simulizi za samaki wa ajabu ambao wanatajwa kuwa na nguvu ya umeme akiwemo samaki anayefahamika kwa jina la Nyika.
Ikumbukwe kuwa maji ya ziwa Tanganyika ni maangavu sana na kuna wakati hukufanya ushawishike kusogea zaidi ingawa ni hatarikutokaa na ziwa hili kuwa na kina kirefu sana.
Pia mbali na makumbusho hayo kuna hifadhi nzuri ya Gombe ambapo utaweza kuwaona Sokwe,meli ya Mv Liemba ambayo inatajwa kuwa meli ya zamani sana ya Kijerumani na inazaidi ya miaka 100 na usisahau kufika mwisho wa Reli(Kigoma Railway station).
Je unapenda kucheza Ngoma za asili? Ukifika Kigoma mjini ulizia ngoma ya Wabembe ni maarufu sana na ambayo huchezwa kwa ustadi mkubwa sana na madoido ya aina yake.
Imeandaliwa na Ng'oko Innocent
Post a Comment