Tangakumekuchablog
Tanga,
KIWANDA
Cha Saruji Cha Simba (Simba Cement) cha Tanga, kimeipa shule ya Sekondari ya
Ilboru Secondary School ya Arusha mifuko 400 ya saruji yenye thamani zaidi ya
milioni 4.8 kwa ujenzi wa vymba vya madarasa.
Akizungumza wakati wa
halfa fupi ya
makabidhiano leo, Mkuu wa Idara ya Rasilimaliwatu kiwanda cha Saruji cha Simba
Cement, Diana Malambugi, alisema msaada huo umetolewa ili kupunguza changamoto
za vyumba vya madarasa kwa shule hiyo.
Alisema msaada huo
utapunguza uhaba
wa vyumba vya madarasa na kutoa wito kutumika kama ilivyokusudiwa na kuiagiza
kamati ya shule kuhakikisha mifuko hiyo inatumika
ipasavyo.
‘Mifuko hii ya saruji
itapunguza changamoto
inayoikabili shule yako ikiwemo vyumba
vya madarasa na ujenzi wa nyumba za walimu, sera yetu moja wapo ni hii ya elimu”
alisema Malambugi
Alimtaka mwalimu huyo
na kamati yake
ya shule kuitunza mifuko hiyo ya saruji na kumhakikishia kuisaidia pale ambapo
kutakuwa na uhitaji na kuwataka wadau wengine wa elimu kusaidia sekta ya elimu
zikiwemo kuondosha changamoto za uhaba wa madawati na vyumba vya
madarasa.
Kwa upande wake,
mwalimu mkuu wa
shule ya Ilboru sekondari school , Julias
Shulla, alikishukuru kiwanda hicho na kusema kuwa msaada huo utatumika kama
ilivyoombwa.
Alisema shule yake
inakabiliana na
changamoto nyingi zikiwemo uhaba wa vyumba vya madarasa pamoja uhaba wa vifaa
vya maabara hivyo kuwataka wadau wa elimu
kuisaidia.
‘Tunakishukuru kiwanda
cha saruji
cha simba kwa moyo wao waliounyesha kwetu, kwa fadhila hii tunawaahidi kuwa
tutaitumia saruji kama tulivyoiomba” alisema
Shulla
Alisema mifuko hiyo
itapunguza kwa
kiasi kikubwa changamoto ambazo shule
yake inakabiliana nazo na kusema kuwa msaada huo ni faraja kwao na wanafunzi wa
shule yake.
Mwisho
Mkuu wa Idara ya
Rasilimawatu
kiwanda cha Sauji cha Simba Cement cha Tanga, Diana Malambugi,
akimkabidhi mifuko
ya saruji 400 yenye thamani zaidi ya milioni 4.8 kwa mwalimu mkuu shule ya
Sekondari ya Ilboru ya Arusha, Julias Shulla ikiwa
ni ujenzi wa vyumba vya madarasa.nyuma
kulia ni Mkuu wa fedha Pieter Jaggar na kushoto ni Emmanuel Jonas
mhasibu.
Mhasibu wa kiwanda cha Saruji cha Simba Cement, Emmanuel Jonas, akimkabidhi mwalimu mkuu wa shule ya Sekondari ya Iboru ya Arusha, Julias Shulla mifuko ya saruji 400 yenye thamani zaidi ya shilingi milioni 4.8 kwa ajili ya ujenzi wa vymba vya madarasa, nyuma ni mkuu wa fedha, Pieter Jaggar.
Afisa Uhusiano kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga, Mtanga Nnour, akimkabidhi mifuko ya saruji 400 yenye thamani zaidi ya shlingi milioni 4.8 kwa mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Ilboru ya Arusha, Julias Shulla, ikiwa ni kusaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa. Nyuma ni mkuu wa fedha, Pietre Jaggar.
Mkuu wa fedha kiwanda cha saruji cha Simba Cement, Pieter Jaggar, akimabidhi mifuko ya saruji 400 yenye thamani zaidi ya shilingi milioni 4.8 mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Ilboru ya Arusha, Julias Shulla ikiwa ni kusaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa, kulia ni meneja usambazaji na ugawaji, Samwel Shoo, nyuma kulia ni Afisa Uhusiano , Nour Mtanga na mkuu wa Idara ya Rasilimawatu, Diana Malambugi.
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Kumekucha. 0655902929
Post a Comment