Raundi
ya tatu ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea
kesho Jumamosi Septemba 3, 2016 kwa michezo minne wakati kwa Jumapili
Septemba 4, mwaka huu kutakuwa na mchezo mmoja tu kwa mujibu wa ratiba
ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliyotolewa na Bodi ya Ligi (TBLB).
Michezo
ya kesho ni kati ya Mbao FC na Mbeya City utakaofanyika Uwanja wa CCM
Kirumba jijini Mwanza wakati Kagera Sugar itazindua uwanja wa nyumbani
kwa kucheza na Mwadui ya Shinyanga.
http://tff.or.tz/news/572-ligi-kuu-ya-vodacom-mechi-nne-kesho
Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini
TAIFA STARS KAZINI KESHO
Timu
ya Mpira wa Miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, kesho Septemba 3, 2016
inatarajiwa kuingia kibaruani kwa kucheza na Super Eagles ya Nigeria
katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi kuwania nafasi ya kucheza
fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2017).
Mchezo
huo utafanyika kuanzia saa 11.00 (17h00) jioni kwenye Uwanja wa
Kimataifa wa Godswill Akpabo, mjini Uyo katika Jimbo la Akwa Ibom. Muda
huo uko mbele kwa saa mbili kamili kwa maana hiyo Taifa Stars itacheza
dhidi ya Nigeria saa 9.00 alasiri (15h00).
MWISHO WA KUJISAJILI GPX NI JUMATATU
Shirikisho
la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), kwa mara nyingine, limeagiza
klabu tisa za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) na Klabu sita za
Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes (TFDL) kujiunga mara moja na mfumo
huo unaoitwa GPX yaani Global Players Exchange ambao malengo yake ni
kurahisisha kufanya usajili kwa mchezaji.
FIFA
imeiandikia barua Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), likitaja
klabu tisa za VPL na TFDL kujisajili kabla ya Jumatatu wiki ijayo kwani
itasaidia kupata taarifa kamili za mchezaji ambayo timu itahitaji
kumsajili. Lengo ni kurahisisha mawasiliano ya usajili kwa mfumo wa
Mtandao (TMS-Transfer Matching System).
Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini
Post a Comment