Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
waTanzania Mama Janeth Magufuli akiongea na Wazee katika makazi ya
Kulea Wazee na watu wenye mahitaji maalum ya Fungafunga yaliyopo
Manispaa ya Morogoro ambapo amezitaka Wizara, Taasisi za Serikali
Mashirika ya ndani na nje ya nchi, watu binafsi na wadau mbalimbali wa
maendeleo wametakiwa kujitokeza katika kuwasaidia wazee na watu wenye
ulemavu ili kuwawezesha kuhakikisha wanapata huduma zote muhimu kwa
kadri iwekenavyo.
Na Hassan Silayo-MAELEZO
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mama Janeth Magufuli amewataka watanzania kumuenzi kwa
vitendo Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa
kuwahudumia Wazee nchini kwa kuwapatia mahitaji ya muhimu kwa ajili ya
ustawi wa maisha yao.
Akiongea na Wazee katika Kambi
ya kulea wazee ya Chazi iliyopo Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro Mama
Janeth amesema kuwa watanzania wanapaswa kutambua Wazee ni kundi muhimu
kwa ustawi wa nchi kwani miongoni mwao walishiriki katika ukombozi wa
taifa leo hivyo tuitumie Siku kama ya leo na nyingine kumuenzi Hayati
mwalimu Julius Nyerere akiwa kama mzee aliyetangulia mbele za haki.
“Leo ni siku muhimu sana katika
taifa letu siku ambayo tunaenzi siku aliyofariki muasisi awa Taifa letu
Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, hivyo ni rai yangu kwa
watanzania kwa ujumla kumuenzi kwa kushiriki kwa pamoja katika
kuwahudumia wazee na kuwapatia mahitaji yao muhimu” Alisema Mama Janeth.
Aidha, Mama Janeth alisema kuwa
amesikia changamoto zinazokabili Makazi hayo na ameahidi kuendelea
kushirikiana na wadau kwa kadri iwezekanavyo ili kuhakikisha wanapunguza
na kuondoa kabisa changamoto hizo iwe makazi ya wazee Chazi na yote
nchini yawe sehemu salama ya kuwahudumia wazee.
Katika kutembelea kituo hicho
Mamam Janeth Magufuli ametoa zawadi ya mchele, Maharagwe,unga na mafuta
ya kupikia kwa ajili ya wazee na watu wasiojiwezakatika kituo hicho.
Akimkaribisha Mgeni Rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe amesema kuwa serikali ya mkoa wake inatekeleza kwa vitendo maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. john Pombe Magufuli ya kuwahudumia wazee na kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ndani mkoa wameshaanza kutatua baadhi ya kero na wataendelea kufanya hivyo ili kuyaimarisha makazi ya wazee mkoani humo.
Akimkaribisha Mgeni Rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe amesema kuwa serikali ya mkoa wake inatekeleza kwa vitendo maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. john Pombe Magufuli ya kuwahudumia wazee na kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ndani mkoa wameshaanza kutatua baadhi ya kero na wataendelea kufanya hivyo ili kuyaimarisha makazi ya wazee mkoani humo.
Pia Dkt. Kebwe amewataka watu
wote waliovamia makazi ya wazee kuondoka mara moja na kutafuta maeneo
mengine na atakayekiuka agizo hilo serikali itamchukulia hatua kali za
kisheria.
Akiwasilisha Risala ya Makazi ya
Ya wazee ya Chazi kwa Mama Janeth Magufuli Kaimu Afisa Mfawidhi wa
Makazi hayo Bw. Richard Kamwana amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa misaada aliyoitoa kwa wazee wa
kituo hicho wakati wa sikukuu ya Eid.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Wilaya ya Mvomero Bw. Florent Kiombo amemuhakikishia Mama Janeth
Magufuli wataendelea kushirikiana na taasisi nyingine katika
kukiendeleza kituo hicho ikiwamo kuwapatia wazee wote kadi za CHF kwa
ajili ya kuwasaidia wazee hao kupata huduma ya Afya popote waendapo.
Post a Comment