Hospitali
ya Taifa Muhimbili imepokea msaada wa mashine kubwa na ya kisasa ya
Utra Sound maalum kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wenye matatizo ya
Figo.
Msaada
huo umetolewa jana na Hospitali ya Chuo Kikuu cha Haukeland cha nchini
Norway ambapo pamoja na mambo mengine wameahidi kuendelea kutoa
ushirikiano katika maeneo ya elimu , utafiti pamoja na vifaa tiba.
Daktari
Bingwa wa magonjwa ya Figo ambaye pia Mhadhiri kutoka MUHAS Paschal
Ruggajo amesema mashine hiyo itasaidia kuchukua sampuli ya figo kwa
ajili ya kugundua magonjwa ya Figo , kuweka vifaa kwenye mishipa damu
kwa wagonjwa wanaoanzishiwa matibabu ya uchujaji wa damu na kugundua
matatizo mbalimbali ya Figo.
“
Kwa muda mrefu sasa tumekua na ushirikiano wa karibu kati ya Hospitali
hiyo , MUHAS na MNH na wametusaidia kufundisha Madaktari sita wa Figo ,
wameshatoa mashine za kusafisha Figo na sasa wametupatia mashine hii
kubwa ya Utra Sound kwakweli tunawashukuru kwa msaada wao.” Amesema Dk. Ruggajo.
Akizungumza
kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili , Dk .
Hedwiga Swai ambaye ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba ameishukuru
Hospitali hiyo ya Haukeland na kusisitiza kuwa msaada huo umekuja
wakati muafaka kwakua mashine hiyo itasaidia sana katika kitengo cha
Figo
Profesa
Einar Svastard ( kulia) akimkabidhi msaada wa mashine kubwa ya
kisasa ya Utrasound Mkurugenzi wa huduma za tiba MNH Dk. Hedwiga Swai
.
Profesa Einar Svastard akimfanyia uchunguzi mgonjwa kwa kutumia mashine hiyo
Post a Comment