Polisi
nchini Kenya katika mji mkuu Nairobi wamemkamata mlinzi wa Benki ya
Equity na kumhusisha na wizi ulifanyika katika mtambo wa kutoa pesa,
ATM. mwishoni mwa juma lilipita na kisha kutoweka. Wezi hao walitoweka
na kiasi cha pesa ambacho hakijajulikana kwa sasa.
Wezi hao walichimba ukuta wa nyuma wa
Benki hiyo na kutoweka na sanduku la uhifadhi wa fedha pamoja na mtambo
mzima wa ATM, huku likiwa na fedha ndani yake.
Inasemekana wezi hao waliweza kuzima kamera za CCTV na pia kengele ya usalama kabla ya kutekeleza wizi huo.
Kamanda wa jimbo la Nairobi Japheth
Koome amesema kwamba polisi walikuta mitungi ya gesi na vifaa vingine
ambavyo hutumuka kukata chuma.
Kamanda alisema inashangaza kuona kwamba
wezi wa siku hizi wanapata maarifa mapya na kufanya matukio utadhani
kwenye filamu na kutadhalisha wizi wa mabenki umeendelea kubadilika kila
siku.
Mwaka uliopita kwenye tukio lingine kama
hilo, wezi walijifanya kama wakaguzi wa hesabu katika benki hiyo
walitoweka na dola za Marekani 300,000.
– BBC/Swahili
Post a Comment