Meya wa jiji la Mbeya David Mwasilindi |
Na JamiiMojablog,Mbeya
Halmashauri
ya jiji la Mbeya imebuni njia mpya ya ukusanyaji wa mapato ili kufikia malengo yake ya ukusanyaji wa kiasi
cha shilingi bilioni 11 katika mwaka
wa fedha wa 2016/17 .
Katika
kufanikisha mpango huo halmashauri imewashirikisha madiwani na wataalmu wake
katika kufanya kazi ya ukusanyaji wa mapato kupitia vyanzo vyake vya ndani .
Moja
ya njia hiyo halmshauri imeanza kuwatumia Madiwani pamoja na wenyeviti wa mitaa
katika ukusanyaji wa fedha kupitia vyanzo vyake vya ndani vya mapato .
Akielezea
mkakati huo Mstahiki Meya wa jiji la
Mbeya Ndugu David Mwashilindi amesema katika kuhakikisha halmshauri inafikia
lengo lake la ukusanyaji wa mapato imeamua kuongeza nguvu kazi kwa kuwaingiza
madiwani na wenyeviti ambao wapo karibu na wananchi.
“ Kazi
kubwa wanayo ifanya madiwani na
wenyeviti kwa kushirikiana na wataalam ni kuhakikisha wanavitambua vyanzo vyote
vya mapato vinavyostahili kuingia katika mapato ya halmashauri ikiwa na kubaini mianya iliyokuwa ikitumiwa na
wahusika kukwepa kulipa kodi,”amesema Mwasilindi.
Amesema
kuziendesha halimamshauri hizi inategemea sana mapato ya ndani hivyo lazima
kuweka jitahada za makusudi katika kufikia malengo husika .
Amesema
katika kipindi cha nyuma halmasahuri hiyo hali ilikuwa katika hali mbaya kwani kwa
mwezi walikuwa wanakusanya kiasi cha shilingi milioni 120 hadi 200 lakini mara
baada ya kuanza kwa jitihada hizo imesaidia kupandisha mapato ambapo kwa sasa
imefikia kiasi cha shilingi milioni 700 kwa mwezi.
Amesema
zoezi hilo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa ambapo sanjali na kukusanya mapato
pia kuna sauala la utoaji wa elimu kwa wananchi ili kuelewa namna ya kulipa tozo zilizo wekwa kisheria.
Amesema
zoezi hilo litadumu kwa muda wa siku tano na mara baada ya hapo kutafanyika kwa
tahimini ya pamoja ili kubaini changamoto zilizopo katika zoezi.
Mwisho.
Post a Comment