Benny Mwaipaja
MAKAMU wa Rais Mama SAMIA SULUHU
HASSAN, amesema kuwa matumizi sahihi ya takwimu zilizokusanywa kwa njia
ya weledi mkubwa yanaweza kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa
kasi zaidi Barani Afrika,
Mama Samia ametoa kauli hiyo leo
wakati akiwatunuku astashada na shahada wahitimu 154 kutoka nchi saba
za kiafrika ikiwemo Tanzania, wakati wa Mahafali ya Pili ya Chuo cha
Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) kilichoko Changanyikeni Jijini Dar
es salaam.
Amewataka wahitimu hao kutumia
elimu na ujuzi walioupata katika chuo hicho kufanya utafiti rasmi na
wenye viwango ili nchi wanachama walioanzisha chuo hicho waweze kutumia
takwimu sahihi kupanga mipango yao ya maendeleo itakayosaidia
kuwaondolea umasikini wananchi wake
Pause Mhe. Samia Suluhu Hassan-Makamu wa Rais-Tanzania
Aidha, amewahakikishia wahitimu
kutoka Tanzania waliomaliza masomo yao katika chuo hicho kwamba serikali
itawapatia ajira ili kuongeza kada ya wasomi waliohitimu mafunzo ya
takwimu rasmi ili kuchochea maendeleo ya nchi
Kwa upande wake, Waziri wa Fedha
na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amesema kuwa Tanzania inatekeleza
Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa ambapo moja ya mambo yatakayosaidia
kufanikisha mpango huo ni matumizi ya takwimu rasmi na sahihi na
kuwataka wahitimu kutoka Tanzania kusaidia kufanikisha nchi kuwa nchi ya
viwanda.
Pause
Mkuu wa Chuo hicho kilichoanzishwa
miaka 51 iliyopita, Profesa Innocent Ngalinda, ameiomba serikali ya
Tanzania na nchi wanachama walioanzisha Taasisi hiyo ya elimu ya juu ya
Takwimu Rasmi, kuijengea uwezo ikiwemo miundombinu ya majengo pamoja na
wakufunzi ili kiweze kuboresha mazingira ya utoaji wa elimu hiyo muhimu
Pause
Akitoa neno la shukurani kwa mgeni
rasmi, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Takwimu ya Taifa Dkt. Albina Chuwa,
amesema serikali imejipanga kutumia wataalamu wa takwimu Rasmi
waliobobea walioko serikalini na katika sekta binafsi kufanikisha
utafiti wa sekta ya viwanda unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
Pause
Wahitimu wa Mahafali ya Pili
katika Chuo hicho cha Takwimu Mashariki mwa Afrika wametoka katika nchi
za Nigeria, Ghana, Ethiopia, Somalia, Uganda, Liberia, Rwanda na wenyeji
Tanzania.