Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali (CAG), Profesa Juma Assad
|
Soko la Mwanjelwa jijini Mbeya |
Na JamiiMojaBlog,Mbeya
MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa
Hesanu za serikali(CAG), anatarajia kuanza kufanya kazi ya ukaguzi maalum
katika halmashauri ya Jiji la Mbeya baada ya kudaiwa kuwepo kwa viashiria vya
ubadhilifu wa fedha zilizotumika kukamilisha ujenzi wa soko la Mwanjelwa.
Awali, Agosti 9 mwaka huu, Waziri
Mkuu Kassimu Majaliwa akiwa katika ziara yake Mkoani Mbeya, alifanikiwa
kutembelea mradi huo wa soko ambao inasemekana umetumia kiasi cha shilingi
Bilioni 26, tofauti na matarajio ya serikali.
Serikali, ilikuwa ikiamini mradi huo
utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 16 lakini kutokana na utendaji kazi wa
hovyo unaodaiwa kufanywa na baadhi ya watendaji tena kwa maslahi yao binafsi
ulisababisha soko hilo kutumia kiasi cha shilingi bilioni 26.
Hatua hiyo ndio iliyomfanya waziri
Mkuu, kumuagiza Mkaguzi Mkuu wa Hsabu za serikali kwenda Mbeya na kufanya
ukaguzi wa mradi huo ili kuondoa utata uliopo juu ya kiasi sahihi cha fedha
kilichotumika kwenye mradi huo.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya, David Mwashilindi |
Akizungumzia hilo, Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya, David Mwashilindi amesema kuwa baada ya agizo la waziri mkuu kutolewa, halmashauri ilianza mchakato wa kumuita mkaguzi huyo ili kufika kufanya ukaguzi.
Amesema, kinachofanyika sasa ni
kamati ya fedha kuketi kwa ajili ya kupitisha matumizi hayo ya fedha na kazi
kuanza kufanyika ikiwa na kutekeleza agizo la Waziri Mkuu.
Amesema Kamati ya fedha inataraji
kukaa November 22 mwaka huu, na kutoa maamuzi na kupitisha kiasi hicho cha
fedha kwa ajili ya kutumika kwa kazi ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ya
kufanya ukaguzi wa fedha katika soko la Mwanjelwa.
Aidha, Meya huyo aliwaomba wafanya
biashara wote ambao tayari waliingia mikataba na halmashauri ya Jiji, kuanza
kuendesha biashara zao kama makubaliano ya mkataba yanavyoelekeza.
Hata hivyo, aliongeza kuwa tayari
halmashauri imeingia mkataba na wakala atakayendesha zoezi la kuwaondoa
wafanyabiashara wote ambao wamekiuka makubaliano ya mkataba kwa kushindwa
kuendesha biashara kwa kipindi husika.
Mwisho.
Post a Comment