Mrembo
wa taji la Miss Tanzania 2010 Genevieve Mpangala amejitosa kusaidia
kurejesha heshima ya mkoa wa Tabora katika elimu hasa kwa wasichana
ambao ndio nguzo kubwa kwa familia na maendeleo ya taifa.
Mrembo
huyo ameamua kufanya hivyo kwa kutembelea shule mbili za Tabora Girls
na Isevya kuongea na wanafunzi, kuwapa moyo na kuangalia matatizo
yanayowasumbua katika kujipatia elimu.
Akizungumza na Moblog
amesema kwamba amekuwa na masikitiko makubwa na matokeo ya mitihani ya
kitaifa ya sekondari kwa miaka mitatu ilhali simulizi za Tabora miaka
iliyopita ni za kufurahisha sana uikionesha kwamba mkoa huo ndio kitovu
hasa cha elimu.
Anasema
ukisoma nyaraka mbalimbali unaona jinsi Tabora ilivyokuwa ngome ya
elimu huku watanzania wengi wakifika hapo pia kupata elimu ya sekondari.
Mrembo wa taji la Miss Tanzania 2010, Genevieve Mpangala akizungumza wa shule ya sekondari Tabora Girls hivi karibuni.
“Kwa
kweli pamoja na masimulizi mazuri kuhusu elimu Tabora miaka ya 80 na 90
,nilichagua Tabora girls kwa sababu ni shule aliyosoma mama yangu mzazi
form 1 mwaka 1977 mpaka 1980 mpaka na aliisifia sana shule yake hiyo na
nikapenda niweze kuwa karibu nao kuhakikisha wanafunzi wote
wanamaliza,na Isevya ilikua chaguo la pili kwasababu ilikua ni shule ya
kutwa (day) na nilipendelea kuongea na wanafunzi hao” alisema Genevieve.
Mkoa
wa Tabora ambao unapatikana kati ya Magharibi ya Tanzania kwenye uwanda
wa latitudo 40-70 Kusini na longitudo 310 – 340 mashariki ukipakana na
mikoa ya Shinyanga, Katavi, Singida, Kigoma na Dodoma ni mji
ulioanzishwa na wafanyabiashara wa Kiarabu kwenye miaka ya 1850
ukijulikana kama Kazeh .
Kihistoria
Kazeh ambayo ilikuwa kitovu cha biashara ya utumwa, mwaka 1871 robo ya
mji ilichomwa moto na kuvurugwa na mtawala wa wanyamwezi Mirambo .
Ingawa
mwaka 1885 hadi 1891 wajerumani walijaribu kutawala, historia zinasema
kwamba mji huo ulikuwa na vurugu kubwa lakini baadae ukatawaliwa na
wajerumani wakafanya mji wa utawala kabla ya vita kuu ya kwanza kuingia
na wao kung’olewa.
Mrembo
wa taji la Miss Tanzania 2010 Genevieve Mpangala akiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya wanafunzi na mwalimu wao alipofanya ziara shuleni
hapo.
Pamoja
na historia yenye misukosuko ya Mkoa wa Tabora ambao ni moja ya mikoa
yenye eneo kubwa unategemea sana kilimo kufanikisha maisha lakini kwa
miaka mingi mkoa umekuwa ukididimia kimaendeleo na kijamii.
Mkoa
wa Tabora ambao umekua wa mwisho kwa miaka mitatu mfululizo mwaka
2013,2014 na 2015 unahitaji nguvu kubwa ya kujiondoa katika shida ya
kuporomoka katika elimu
Mrembo
Genevieve anasema ziara yake katika shule hizo imemfumbua macho na
kuona haja kubwa ya kuendelea na programu za kufufua matumaini.
Pamoja
na kuwashukuru walimu kwa ushirikiano waliompa aliwataka wanafunzi
kuweka mkazo katika imani, matumaini na kutekeleza ndoto zao katika
uwanda mkubwa zaidi.
Aidha
pamoja na kuzungumza “HAVE FAITH,HOPE FOR MORE AND DREAM EVEN BIGGER”,
pia aliwaasa kuwa elimu ni msingi mzuri wa maisha na kuwa wasiharakishe
na kupotoshwa na mambo ya kidunia kwani haya maisha yapo.
Akiwa
na wasichana wa shule ya Tabora Girls walimweleza changamoto
wanazokutana nazo ikiwa ni pamoja na kutokuwepo na uzio kwenye shule yao
hiyo, uhaba wa vitabu, upungufu wa walimu, uhaba wa upatikanaji wa
habari mubashara, kwa wanafunzi kwamba hawana king’amuzi,kwa wanafunzi
wenye ulemavu wa ngozi wanauhitaji wa msaada wa kofia pamoja na mafuta
ya kuwakinga na jua.
Matatizo
hayo yanatokana zaidi na kwamba wengi wao wanatoka kwenye mazingira
duni. Changamoto nyingine ni pamoja na kuwa na zahanati ambayo ina uhaba
wa vifaa mfano:vyandarua vya kutosha pamoja na vitanda,pia kwa
wanafunzi ambao wanaulemavu wa macho ambao ni hafifu na vipofu kabisa
hivyo kuna uhaba wa brail paper.
Ziara
fupi ya Mrembo wa Tanzania 2010 Genevieve Mpangala kwa shule mbili za
jijini Tabora za Isevya Secondary School na shule ya vipaji maalum ya
wanawake Tabora girls.
Amesema
katika mazungumzo yake na wanafunzi hao amebaini pia kwamba kutofanya
vyema kwa wanafunzi pia kunasababishwa na wanafunzi hao kutumia madawa
ya kulevya, utoro, mimba za shuleni na wazazi kuozesha mabinti katika
umri mdogo kabla ya wao kumaliza shule.
Post a Comment