Wananchi
wakiangalia ajali iliyohusisha magari manne na pikipiki iliyotokea
daraja la Mzinga Kongowe, Temeke jijini Dar es Salaam leo mchana. Katika
ajali hiyo watu kadhaa walijeruhiwa.
Wananchi wakiangali basi dogo aina ya Coster ya abiria namba T 415 DCC ikiwa imeharibika vibaya baada ya kugongwa.
Wananchi wakiwa eneo la ajali
Wananchi wakiwa eneo la ajali.
Ofisa wa Jeshi la Polisi akiwa eneo la ajali akichukua taarifa.
Prado yenye namba T 177 AHH iliyohusika katika ajali hiyo.
Na Dotto Mwaibale
WATU
kadhaa wamejeruhiwa vibaya katika ajali iliyohusisha magari manne na
pikipiki iliyotokea daraja la Mzinga Kongowe Manispaa ya Temeke jijini
Dar es Salaam.
Ajali
hiyo ilitokea saa sita mchana na kuhusisha magari hayo lori la mafuta
aina ya Scania lenye namba T 617 AQQ, Coster ya abiria namba T 415 DCC
inayofanya safari zake kati ya Kilwa Masoko na Mbagala, Prado yenye
namba T 177 AHH, pikipiki na lori jingine.
Ofisa
wa Polisi aliyekuwepo eneo la ajali ambaye alitambulika kwa jina moja la
Emanuel alisema chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika.
“Nimefika sasa hivi bado hatujajua chanzo cha ajali wala watu waliopoteza maisha na kujeruhiwa” alisema ofisa huyo.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Temeke, Gilles Muroto alipopigiwa simu ili
kuthibitisha ajali hiyo alikiri kutokea hata hivyo alisema alikuwa
hajapata taarifa kamili kutoka kwa Mkuu wa Kikosi cha Usalama wa Wilaya
hiyo ambaye alikuwepo eneo la tukio.
Kwa mujibu wa mashuhuda walioshuhudia ajali hiyo walisema majeruhi walikimbizwa Hospitali ya Manispaa ya Temeke kwa matibabu.
Post a Comment