Diwani
wa kata ya Mchikichini, Joseph Ngowa (katikati), akihutubia wakati
akizindua kampeni ya siku 16 ya kupinga ukatili wa kijinsia
iliyoandaliwa na Shirika la Eguality for Growth (EfG), Dar es Salaam leo
asubuhi.Kushoto
ni Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Wanawake katika Soko la Mchikichini,
Betty Mtewele na kulia ni Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mchikichini, Charles
Kapongo.
Ofisa Ufuatiliaji na Tathmini wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Shabani Rulimbiye (kulia), akitoa
taarifa fupi kuhusu kampeni hiyo mbele ya mgeni rasmi kwa niaba ya
Mkurugenzi Mtendaji wa EfG, Jane Magigita. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti
wa Wafanyabiashara Wanawake katika Soko la Mchikichini, Betty Mtewele,
Diwani wa kata hiyo, Joseph Ngowa na Ofisa Mtendaji wa Kata ya
Mchikichini, Charles Kapongo.
Ofisa
Ufuatiliaji na Tathmini wa Shirika la Equality for Growth (EfG),
Shabani Rulimbiye (kushoto), akipeana mkono na mgeni rasmi baada ya
kumkabidhi risala.
Mjumbe wa Soko la Mchikichini, Victor Kalokola akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Msaidizi
wa kisheria masokoni, Irene Daniel akitoa ushuhuda wa hatua
zilizochukuliwa kwa baadhi ya watu waliobainika kujihusisha na vitendo
vya ukatili wa kijinsia katika Soko la Tabata Muslimu.
Mwenyekiti wa Wanawake Wafanyabiashara katika Soko hilo, Betty Mtewele (kushoto), akisisitiza jambo kwenye uzinduzi huo.
Wananchi waliohudhuria uzinduzi huo.
Wadau wa EfG wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Wadau wa EfG wakiwa wakiwa katika picha ya pamoja mgeni rasmi wa Diwani wa Kata ya Mchikichini, Joseph Ngowa (kushoto)
Diwani
wa Kata ya Mchikichini, Joseph Ngowa (kushoto), akigawa vipeperushi vya
kupinga ukatili wa kijinsia kwa wafanyabiashara wa soko la Mchikichini.
Wasanii wa kundi la machozi wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Wasanii
wa Kikundi cha Machozi wakitoa burudani kwenye uzinduzi wa kampeni ya
siku 16 ya kupinga ukatili wa kijinsia ulioandaliwa na Shirika la
Equality for Growth (EfG) uliofanyika Soko la Ilala Mchikichini Dar es
Salaam leo.
Uzinduzi ukiendelea
Wasaidizi wa kisheria masokoni, Aisha Juma (kushoto) na Irene Daniel wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Usikivu kwenye uzinduzi huo. Katikati ni Msaidizi wa kisheria masokoni Batuli Mkumbukwa.
Picha ya pamoja na mgeni rasmi Diwani wa Kata ya Mchikichini, Joseph Ngowa.
Na Dotto Mwaibale
DIWANI
wa Kata ya Mchikichini Joseph John Ngowa (Chadema), amemfutia leseni ya
biashara, Alex Richard muuza mitumba katika Soko la Karume Ilala jijini
Dar es Salaam baada ya kumbamba akimfanyia udhalilishaji mteja wake wa
kike.
Tukio
hilo limetokea Dar es Salaam leo mchana wakati Diwani huyo alipokuwa
akienda kugawa vipeperushi vya kupinga ukatili wa kijinsia kwa
wafanyabaiashara wa soko hilo baada ya kuzindua kampeni ya siku 16 ya
kupinga ukatili wa kijinsia iliyoanzishwa na Shirika la Equality for
Growth (EfG) ndipo alipoingia kwenye kibanda cha mfanyabiashara huyo na
kumkuta mteja wa kike akiwa ametoa nguo zake akipimishwa nguo za mitumba
kitendo ambacho ni ukiukaji wa sheria ndani ya soko hilo.
“Kuanzia
leo hii naagiza ufutiwe leseni yako ya biashara kutokana na tukio ili
la aibu na kidhalilishaji ili iwe fundisho na kwa wengine” aliagiza
Ngowa.
Ngowa
alitishia kuwafuti leseni za biashara wafanyabiashara watakaobainika
kuwadhalilisha wateja wao hasa wanawake na kuwa wanamsaka kijana moja
maarufu kwa jina la Kipracheche ambaye ni kinara wa ubakaji na
kudhalilisha wanawake katika soko hilo ikiwa ni pamoja na
kulisambaratisha kundi la kihalifu sokoni hapo linalojulikana kwa jina
la Masabanga.
Mfanyabiashara
huyo Alex Richard alipohojiwa na wanahabari kuhusu vitendo hivyo
aliomba samahani na kuwataka wenzake waache kufanya vitendo hivyo vya
udhalilishaji kwa wanawake.
Mwenyekiti
wa Wanawake Wafanyabiashara katika Soko hilo, Betty Mtewele alisema
mfanyabiashara yeyote atakaye bainika kujihusisha na vitendo vya
udhalilishaji wa kijinsia hata unewa huruma atachukuliwa hatua kazi za
kisheria.
Akizungumza katika uzinduzi huo Ofisa Ufuatiliaji na Tathmini wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Shabani Rulimbiye alisema
katika vitendo vya kupinga ukatili wa kijinsia shirika hilo linaendesha
mradi unaoitwa “Mpe Riziki si Matusi” katika Wilaya ya Ilala na Temeke
katika masoko sita ambayo ni Mchikichini, Kisutu, Tabata Muslimu, Ferry,
Gezaulole na Temeke Sterio lengo likiwa ni kuona wanawake
wafanyabiashara wa Manispaa ya Ilala na Temeke wanafanyabiashara zao
katika mazingira huru dhidi ya ukatili wa kingono, kimwili, matusi na
kisiasa, vilevile kuona wanawake wakipewa heshima kama binadamu wengine
ili waweze kujipatia kipato chao bila vikwazo.(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)
Post a Comment