Watazamaji wa anga wanajiandaa kuuona mwezi mkubwa zaidi wakati ambapo utakaribia dunia tangu 1948.
Uingereza
itakuwa na fursa nzuri kuuona mwezi huo siku ya Jumatatu jioni,licha ya
kuwa utakaribia dunia mwendo wa saa tano na dakika 21 muda wa GMT
ambapo utakuwa umbali wa kilomita 356,509.
Wachunguzi watauona
mwezi huo kuwa mkubwa zaidi kwa asilimia 7 ukilinganishwa na mwezi wa
kawaida na kung'aa zaidi ya asilimia 15, licha ya kwamba macho ya
binaadamu yanaweza kupambanua tofauti hiyo.
Huku mwezi huo
ukitarajiwa kutokaribia dunia hadi tarehe 25 mwezi Novemva 2034, idara
ya maswala ya hewa nchini Uingereza imesema kuwa kutakuwa na mawingu
mazito wakati mwezi huo utakapokaribia.
Huku mwezi ukizunguka
dunia,kuna tofauti ya mwangaza unaotolewa na jua.Ni wakati huo ambapo
mwezi wote humulikwa na mwangaza huo na kutoa mwezi mkubwa zaidi.BBC |
Post a Comment