Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya
limewafukuza kazi askari wake wawili kutokana na kuwafanyia vitendo
vinavyokwenda kinyume cha maadili wanafunzi wa kike wa kidato cha nne
katika shule ya Sekondari ya Isuto Kata ya Isuto, Wilaya ya Kipolisi
Mbalizi.
Kwa
mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya Naibu Kamishna wa Polisi
Dhahiri Kidavashari amewataja askari waliofukuzwa kazi kuwa ni H.4925 PC
Petro Oscar Magana wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoa wa Mbeya na
J.1422 PC Lucas Joseph Ng’weina wa Wilaya ya Kipolisi Mbalizi.
Kamanda Kidavashali amesema mnamo Novemba 4 mwaka huu majira ya saa 5:30 Usiku huko katika Shule ya Sekondari Isuto iliyopo Kijiji na Kata ya Isuto, Tarafa ya Isangati, Wilaya ya Kipolisi Mbalizi, Mkoa wa Mbeya, askari hao wawili wawili wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya walituhumiwa kuwafanyia vitendo vibaya kinyume na maadili wanafunzi wa kike wa kidato cha nne wa Shule hiyo wanaoendelea na mtihani wa Taifa.
Amesema kuwa, askari hao kwa pamoja wakiwa kwenye ulinzi wa mitihani ya kitaifa ya kidato cha nne 2016 waliwatoa kwenye Hostel wanafunzi wa kike kwa kile walichodai kupiga kelele.
Amesema baada ya kuwatoa wanafunzi hao, waliwapeleka eneo la kufoleni na kuanza kuwapa adhabu mbalimbali ambazo ni kupiga push up, kuruka kichura, kushika masikio na kuwachapa viboko sehemu za makalio vitendo vilivyowasababishia maumivu makali na kupelekea baadhi ya wanafunzi hao wa kike kuondoka na kurudi majumbani kwao”.
Amesema Kufuatia vitendo hivyo, Mkuu wa Shule hiyo, Rose Dihembe alitoa taarifa kwa uongozi wa Wilaya ambapo taarifa zilifika kwa uongozi wa Mkoa ambao mara moja walifika eneo la tukio na kuchukua hatua za awali ikiwemo kusikiliza malalamikio hayo ya tukio na kuwaondoa askari waliolalamikiwa na mwisho kuchukua hatua za kinidhamu zilizopelekea kufukuzwa kazi askari hao.
Hata hivyo kamanda Kidavashari amesema kutokana na vitendo walivyovifanya askari hao jeshi la polisi linatarajia kuwafikisha mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika.
Kamanda huyo, ametoa wito kwa wananchi mkoani hapa kuendelea kuliamini Jeshi la Polisi na kwamba halitafumbia macho vitendo vya askari vinavyokwenda kinyume na maadili ya kazi yao na pia kinyume na sheria za nchi.
Aidha Kamanda Kidavashari ameomba wananchi kuendelea kutoa taarifa ya vitendo vyote vya uhalifu vinavyotendwa bila kujali vinatendwa na askari au wananchi wa kawaida ili hatua kali za kisheria ziweze kuchukuliwa.

Post a Comment